Afisa mwandikishaji jimbo la Geita na Busanda Bi Sarah Yohana Agosti 2, 2024 amefungua mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kwa waendesha bvr na waandikishaji wasaidizi jimbo la geita wapatao 446 katika ukumbi wa shule ya sekondari bugando.
Bi Sarah amewataka maafisa hao kufanya kazi kwa uaminifu ili zoezi hilo liende kama lililovyokusudiwa.”Kila mtu ameaminiwa na Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi kwamba anaweza kufanya zoezi la uboreshaji wa daftari la mpiga kura” amesema Bi Sarah.
Maafisa waandikishaji wasaidizi na waendesha bvr jimbo la geita wakiwa katika mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga kura katika ukumbi wa shule ya sekondari Bugando.
Jumla ya vituo 490 katika jimbo la Busanda na Geita Vijijini vitatoa huduma ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura zoezi ambalo litaanza Agosti 5, 2024 na kumalizika Agosti 11, 2024
Kwa mujibu wa Kanuni za 46, 47, 48, 49, 50 na 51 (1) za Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2024 zilizoandaliwa chini ya Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Na. 1 ya Mwaka 2024 Watazamaji wa ndani na kimataifa, wanaruhusiwa kutazama mchakato wa Uboreshaji utakavyofanyika katika vituo vya Uandikishaji.
Watazamaji wa Uandikishaji kabla ya kuanza kutembelea vituo vya Uandikishaji, ni lazima waombe na kupatiwa idhini ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Watazamaji.
Afisa Mwandikishaji Msaidizi Jimbo la Geita Mwl Paul Magubiki(wa kwanza kulia) akisaidiana na maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata jimbo la Geita akifuatilia Uendeshaji wa mashine za BVR ngazi ya Kituo katika mafunzo yaliyofanyika ukumbi wa shule ya Sekondari Bugando
Aidha, Watazamaji 24 watakaoruhusiwa na Tume watapewa barua za kuwatambulisha kwa Maafisa Waandikishaji na Mwongozo wa watazamaji wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ulioandaliwa na Tume.
Maafisa Waandikishaji watatakiwa kuwapa barua za kuwatambulisha kwa Watendaji wa vituo ambavyo watavitembelea. Aidha, Watazamaji wa Uandikishaji wa Wapiga Kura hawapaswi kutoa maelekezo kwa Mwandishi Msaidizi katika kituo husika.
Zoezi la uboreshaji wa wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura lilizinduliwa rasmi Jumamosi, Julai 20, 2024 katika uwanja wa Kawawa, mkoani Kigoma na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) huku kauli mbiu ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ikisema Kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora.
Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Mpiga kura yaliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Bugando Agosti 2 na 3, 2024.Maafisa hao wameaswa kufanya kazi kwa uaminifu ili zoezi hilo liende kama lililovyokusudiwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa