Hayawi hayawi hatimaye yamekuwa baada ya mchakato mrefu katika mbio za uchaguzi wa viongozi ngazi ya Serikali za Mitaa leo Novemba 29, 2024 viongozi waliochaguliwa na wananchi kuongoza Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Kufuatia uchaguzi uliofanyika Novemba 27, 2024 wamekula kiapo cha uaminifu na kutunza siri, utii na uadilifu mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Nyarugusu Mhe Joseph P Kaguli.
Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Nyarugusu Mhe Joseph P Kaguli akiwaapisha Viongozi waliochaguliwa kuongoza Serikaliy za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Uapisho huo umefanyika katika ukumbi wa Amani na Upendo Kata ya Nyarugusu ambapo viongozi kutoka kata za Nyarugusu, Nyaruyeye, Nyakamwaga Rwamgasa na Busanda wamekula kiapo hicho ambapo Mhe Kaguli Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo amewataka viongozi walio kula kiapo kutokufanya mzaha na kiapo hicho katika kuwatumikia wananchi.
Viongozi waliochaguliwa na wananchi kuongoza Serikali za Mitaa wakila kiapo cha utii uadilifu na kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Nyarugusu Mhe Joseph P Kaguli
Viongozi wa Serikali za Mitaa wakila kiapo cha utii, uadilifu na kutunza siri Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Muchunguzi Mujuni katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Bugando
Akifungua kikao hicho cha kuwaapisha Viongozi hao Msimamizi Msaidizi ngazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi Sarah Yohana amewapongeza viongozi hao kwa kupewa dhamana ya kuwatumikia wananchi na kuwataka kuwa chachu ya kuendelea kuchochea shughuli za maendeleo.
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Geita Bi Sarah Yohana akiwaasa Viongozi waliochaguliwa kuongoza Serikali za Mitaa Wakati wa Kiapo kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Amani na Upendo Kata ya Nyarugusu
Zoezi la uapisho limefanyika katika maeneo mbalimbali Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo viongozi kutoka kata za Katoro, Nyamigota, Ludete, Magenge na Kaseme wameapa mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Katoro Mhe Adam W.Mashiba.
Kwa upande wa viongozi kutoka kata za Nzera, Katoma, Izumacheli, Nyamboge,Lwezera,Nkome, Kakubilo, Bugulula, Senga na Nyawilimilwa wamekula kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mahakama ya Wilaya ya Geita Mhe Muchunguzi Mujuni.
Viongozi waliochaguliwa kuongoza Serikali za Mitaa Novemba 27,2024 wakila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Katoro Mhe Adam W.Mashiba Kata ya Katoro
Zaidi ya Viongozi 1657 wamekula kiapo leo katika maeneo tofauti ambapo wasimamizi wasaidizi wamewapongeza na kuwatakiwa majukumu mema katika majukumu yao ya kuwatumikia wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa