OCTOBA 5, 2024 Halmashauri ya Wilaya ya Geita inatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru ambao utakimbizwa umbali wa km 45 kutoka eneo la mapokezi kata ya Bugulula hadi eneo la mkesha katika kata ya Nkome na km 34 kutoka kata ya Nkome hadi makabidhiano katika halmashauri ya Buchosa wilaya ya Sengerema Mkoa wa Mwanza na kufanya jumla ya km 79.6.
Katika kuhakikisha maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yanakuwa mazuri, kamati kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita ikiongozwa na Afisa mipango wa Mkoa wa Geita Ndg.Deodatus Kayango Julai 25, 2024 imefanya ziara ya kukagua miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ifikapo October 5,2024.
Timu ya Ukaguzi wa miradi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita ikikagua miradi ya maendeleo inayotarajiwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru Octoba 05, 2024 katika halmashauri ya Wilaya ya Geita Julai 25, 2024. Huu ni mradi wa shamba la miti unaomilikiwa na mtu binafsi. Shamba hilo lina ukubwa wa ekari 6 ambapo ekari 5 ndizo zimepandwa miti aina ya Pinus Caribea. Kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru inasema “TUNZA MAZINGIRA NA SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA UJENZI WA TAIFA ENDELEVU”
Kamati hiyo imezunguka katika miradi yote ambayo Mwenge wa Uhuru utakimbizwa ambayo ni Kata za Bugulula Mwenge wa uhuru utakapo pokelewa na kisha kuendelea katika kata za Nzera, Katoma,Nyamboge na mwisho kata ya Nkome ambapo kutakuwa na mkesha wa Mwenge wa Uhuru.
Mradi wa Maji kata ya Katoma wenye tanki lenye ujazo wa lita 225,000 ambapo unatarajiwa kutoa huduma kwa wakazi wapatao 11,609 kupitia vituo vya kuchotea na wateja wa majumbani
Mbio za Mwenge wa Uhuru zinatarajiwa kukagua miradi mbalimbali itakayozinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi zikiwemo shule, zahanati,ofisi, miradi ya maji, barabara pamoja na klabu za kuzuia na kupambana na rushwa na dawa za kulevya.
Ukaguzi wa mradi wa barabara ya Lami nyepesi yenye urefu wa km 1.1 unaojengwa na TARURA
Aidha katika ukaguzi wa miradi hiyo Kayango amewasisitiza wahandisi na mafundi ujenzi wanaotekeleza miradi hiyo kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na weledi ili kujenga miradi iliyo bora na kuepuka kujenga miradi iliyo chini ya kiwango.
Ukaguzi wa mradi wa zahanati ya Nkome. Timu hiyo imemtaka Mkandarasi kuongeza kasi ya ukamilishwaji wa mradi huo kwa kuhakikisha mafundi wanakuwa katika eneo la ujenzi (site)
Vilevile Kayango amewataka watendaji wa kata zote Mwenge wa Uhuru utapopita kuendelea kufanya hamasa ili wananchi wajitokeze kwa wingi katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru.
Kikundi cha vijana (Masakuro) kata ya Nyamboge wanaoendesha mradi wa kukodi baiskeli ulioanzishwa kwa nguvu ya vijana na kuungwa mkono na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kupatiwa mkopo wenye riba nafuu ambapo kamati hiyo imekipongeza na kukitaka kuendelea kujituma kwa bidii zote ili kuweza kufikia malengo yao.
Mbali na hivyo kamati hiyo imekipongeza kikundi cha vijana (Masakuro) kata ya Nyamboge wanaoendesha mradi wa kukodi baiskeli ulioanzishwa kwa nguvu ya vijana na kuungwa mkono na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kupatiwa mkopo wenye riba nafuu.
“Muendelee kujituma kwa bidii zote ili kuweza kufikia malengo yenu na mnapokamilisha mkopo wenu muendelee kukopa ili kukuza kikundi chenu”,amesema Kayango
Kikundi hicho kimeishukuru halmashauri kwa kuwapa mkopo na kuahidi kuendelea kuchapa kazi pasipo kuchoka na kuweza kupata kile walichokusudia.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa