Geita
TIMU ya mpira wa miguu Halmashauri ya wilaya ya Geita Septemba 7, 2024 imepokea zawadi ya shilingi milioni 2 na laki 5 baada ya kuibuka kuwa mshindi katika mashindano ya Michezo ya Watumishi wa Mamlaka za Serikali za mitaa Tanzania ( Shimisemita) mwaka 2024 yaliyoanza Agosti 24 na kumalizika Septemba 5,2024 katika Jiji la Mwanza.
Kikosi cha mpira wa Miguu halmashauri ya wilaya ya Geita kilichobeba ushindi baada ya kuibuka washindi wa mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano ya Shimisemita yaliyofanyika uwanja wa nyamagana Mwanza na kufanikiwa kuicharaza timu ya Ifakara TC magoli mawili kwa moja.
Mapokezi ya timu hiyo yamefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kilimanjaro iliyopo Geita na kuhudhuriwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Geita Mh Hashim Abdallah Komba, watumishi na wakuu wa idara na vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Geita pamoja na aliyekuwa mmoja wa wadhamini wa timu hiyo benk ya CRDB-Geita.
Kikosi cha mpira wa Miguu halmashauri ya wilaya ya Geita kilichobeba ushindi baada ya kuibuka washindi wa mchezo wa mpira wa miguu katika mashindano ya Shimisemita yaliyofanyika uwanja wa nyamagana Mwanza na kufanikiwa kuicharaza timu ya Ifakara TC magoli mawili kwa moja.
Akizungumza katika Halfa hiyo wakati wa kukabidhi kitita hicho, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Rajab Magaro amewataka washiriki hao kuendelea kuhamasishana iliwatumishi wenye vipaji waendelee kujitokeza na kuendelea kufanya maandalizi mazuri ili kupata vikombe vingi vya ushindi mwakani mashindano hayo yatakapofanyika katika jiji la Tanga.
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakiwa katika picha ya pamoja katika halfa iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Kilimanjaro ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya Halmashauri baada ya kuchukua kombe la ubingwa mashindano ya Shimisemita jijini Mwanza.
Timu ya menejimenti ya Halmashauri ya wilaya ya Geita (CMT) imetoa kitita cha shilingi Milioni mbili na laki tano kama sehemu ya pongezi kwa wachezaji hao ili kuendelea kuwatia moyo wa kushiriki mashindano mbalimbali na kuendelea kuleta ushindi katika halmashauri ya Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Komba akimvalisha medali ya ushindi Mkuregenzi Mtendaji ndg Karia Rajab Magaro katika halfa iliyofanyika hoteli ya Kilimanjaro Geita
Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba amempongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa kupeleka timu kushiriki mashindano ya Shimisemita na kurudi na ushindi.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndg Karia Magaro amekabidhi kiasi cha shilingi 2,500,000 kwa kikosi cha ushindi mashindano Shimisemita katika halfa iliyo andaliwa na menejimenti (CMT) ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Mhe Komba amewataka watumishi hao walioshiriki mashindano ya Shimisemita kuendelea kumuunga mkono Mkurugenzi kuhakikisha kazi zake zote za Halmashauri zinaenda vizuri kwa kuendelea kufanya kazi kwa upendo na watumishi wa umma ili kuendelea kuwa na matokeo mazuri.
Kikosi hicho kilitia kambi jijini Mwanza Agosti 24 hadi mashindano hayo yalipofungwa Septemba 5, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Said Mtanda kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Maafisa Michezo na Maafisa Utamaduni wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu katika halfa ya kuwapongeza wachezaji wa timu ya halmashauri ya wilaya ya Geita iliyofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa