Nzera-Geita.
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilayani Geita unatekeleza miradi ya mtandao wa barabara wenye jumla ya Km 1,745.79.
Akizungumza Februari 04, 2026 wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya pili Oktoba hadi Desemba katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri uliopo Nzera Mhandisi Bahati Subeya ambaye ni Meneja Wilaya amesema TARURA inatekeleza Mradi wa Barabara ndani ya Halmashauri ambapo lami ni Kilometa 5.60, barabara za Changarawe kilometa 726.69, barabara za Udongo Kilometa 1012.055 na Madaraja 638 na kufanya Jumla ya Kilometa 1745.785.
Mhandisi Subeya amesema Halmashauri ya Wilaya ya Geita inachangia kiasi cha Shilingi Milioni 600 kupitia mapato yake ya ndani huku kiasi kingine kikitoka Mfuko wa barabara Shilingi Bilioni 1.8, majimbo Bilioni 1.5 na Tozo Bilioni 3.5.
Pamoja na hayo Mha Subeya amewataka wananchi kuacha tabia ya kupitisha mifugo barabarani inayopelekea kuharibika kwa barabara, pamoja na kukemea wizi wa alama na miundombinu ya barabara na kuepuka kuziba mifereji ya kutoa maji ya mvua mara tu matengenezo ya barabara yanapokamilika.
Vilevile Mha Subeya amesema yapo mabadiliko ya sheria ambayo yatapelekea kuwa na matumizi sahihi ya barabara ili kuendelea kuzilinda.
“Sheria hizi zinazuia matumizi ambayo sio sahihi pamoja na kufanya shughuli ambazo hazina vibali kufanyika katika miundombinu ya barabara kama vile uingizaji wa mifugo maeneo ya barabara, magari yenye uzito mkubwa hasa maeneo yenye shughuli za uchimbaji” Amesema Mha. Subeya.
Ukamishaji wa miundombinu hiyo ya barabara utaendelea kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi ndani ya Halmashauri na nje ya Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa