Na: Hendrick Msangi
Wakala wa barabara za Vijijini na Mijini Tanzania (TARURA), May 9, 2024 imewasilisha taarifa yake ya utekelezaji wa shughuli za serikali ngazi ya Halmashauri na taasisi kwa kipindi cha robo ya tatu Januari hadi Machi 2024 katika Kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Akiwasilisha taarifa ya TARURA kwenye Baraza hilo, Injinia Jerry Mwakapemba amesema barabara nyingi zimeharibika kutokana kiwango kikubwa cha mvua zinazonyesha nchini ikiwa ni pamoja na kukwamisha kazi za ujenzi wa barabara na kupeleka kupunguza kasi ya kukamilisha miradi kwa wakati.
Injinia Mwakapemba amewata wananchi wananchi kuacha kuziba mifereji ya kutolea maji ya mvua ili kuendelea kuilinda miundombinu ya barabara pindi matengenezo yanapokamilika.
Wakala wa Barabara za vijijini na Mjini Wilaya ya Geita inahudumia mtandao wa barabara za wilaya (collector, feeder and community Roads) wenye jumla ya Km 2969.01 sawa na km 1745.79 Halmashauri ya Wilaya na km 1223.22 Halmashauri ya Mji.
Katika taarifa yake Injinia Mwakapemba amesema hadi kufikia mwezi Machi 2024 jumla ya shilingi 1,546,545,387.92 zimepokelewa kutoka vyanzo mbalimbali ambavyo ni mfuko wa barabara, majimbo, tozo ya mafuta na mapato ya ndani toka Halamashauri ya Wilaya ya Geita.
Jumla ya km 1745.79 za barabara ndani ya halmashauri ya wilaya ya Geita zinahudumiwa na wakala wa barabara za vijijini na mjini ambapo kati ya kilometa hizo barabara za lami ni kilometa 4.2, barabara za changarawe ni kilometa 655.07 wakati barabara za udongo ni kilometa 1086.52 na madaraja 518.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa