• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

SERIKALI KUGAWA BILA MALIPO VYANDARUA 539,210 VYENYE VIUATILIFU VYA MUDA MREFU KWENYE KAYA ZOTE-GEITA DC

Posted on: August 5th, 2024

Jumla ya vyandarua 539,210 vyenye viuatilifu vya muda mrefu vinatarajiwa kugawiwa kwenye kaya zote katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ili kuhakikisha maambukizi ya Malaria yanapungua kwenye Mkoa wa Geita ambao kitaifa unashika nafasi ya tano katika maambukizi ya Malaria.

Hayo yamelezwa Agosti 1, 2024 katika semina ya uhamasishaji wa viongozi na mafunzo kwa watendaji ngazi ya mkoa na Halmashauri juu ya kampeni  ya ugawaji wa vyandarua kwenye jamii (kaya) Mkoa wa Geita iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita  ambayo imeratibiwa na Wizara ya Afya na  OR-TAMISEMI ikishirikiana na Johns Hopkins Center for Communication Programs (JHUCCP) kupitia mradi wa PMI Vector Control Activity chini ya ufadhili wa Mfuko wa Rais wa Marekani (USAID) wa kupambana na Malaria.

Maafisa Kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Kaimu Katibu tawala Wilaya ya Geita Bi Janeth Mobe wakiwa na wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita  waliposhiriki semina ya uhamasishaji wa viongozi na mafunzo kwa watendaji ngazi ya Halmashauri juu ya kampeni  ya ugawaji wa vyandarua kwenye jamii (kaya) iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita  ambayo imeratibiwa na Wizara ya Afya na  OR-TAMISEMI ikishirikiana na Johns Hopkins Center for Communication Programs (JHUCCP) kupitia mradi wa PMI Vector Control Activity chini ya ufadhili wa Mfuko wa Rais wa Marekani (USAID) wa kupambana na Malaria.

Kufuatia taarifa ya Malaria ya dunia ya mwaka 2023, imeonyesha  kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wa malaria kutoka wagonjwa  Milioni 244 mwaka 2021 hadi kufikia  wagonjwa  milioni  249 mwaka 2022  huku vifo vitokanavyo na Malaria vikipungua kutoka 610,000 hadi vifo 608,000 mwaka 2021 na 2022 na kueleza kuwa kati ya wagonjwa wote asilimia 93.6 ya vifo vimetokea barani Afrika huku ikikadiriwa kuwa asilimia 93 ya Watanzania wanaishi katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa Malaria.

Katika kutekeleza azma ya kupambana na ugonjwa wa Malaria kampeni ya TMC (Targeted Mass Campaign) imelenga kutekeleza majukumu tofauti tofauti ikiwemo uhamasishaji wa viongozi ngazi ya Mkoa na Halmashauri kusajili kaya kwa mfumo wa ki-elektroniki kwa ajili ya kupatiwa vyandarua, ugawaji wa vyandarua vilivyoainishwa kwa watendaji wa vijiji au mitaa pamoja na uhamasishaji juu ya matumizi sahihi na utunzaji wa vyandarua.  

Washiriki wakifuatilia semina juu ya kampeni ya ugawaji wa vyandarua vyenye viutilifu kwenye jamii (kaya) katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo jumla ya vyandarua 539,210 vyenye viuatilifu vya muda mrefu vinatarajiwa kugawiwa bila malipo  kwenye kaya zote katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita  

Akitoa semina hiyo Afisa Uhamasishaji Ndg Didas Misana kutoka Wizara ya Afya kitengo cha Kupambana na Ugonjwa wa Malaria amesisitiza elimu itolewee kwa jamii kuepukana na imani potofu juu ya vyandarua vinavyotolewa na kuvitumia kujikinga na mbu waenezao Malaria bila kuwa na wasiwasi wowote.

Pamoja na hayo jamii na viongozi wa dini wameaswa kuendelea kuihamasisha jamii juu ya zoezi la ugawaji wa vyandarua katika kaya zao na kuhimiza matumizi sahihi ya vyandarua sambamba na kutoa hamasa juu ya matumizi ya vyandarua na kutokomeza mila potofu juu ya matumizi ya vyandarua kwenye jamii ili kuendelea kuongeza umiliki wa vyandarua kwenye kaya na kufikia lengo la Shirika la Afya Duniani (WHO) la umiliki wa >80% (Chandarua kimoja kwa watu wawili)

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC KOMBA ARIDHISHWA NA UTEKEKEZAJI WA MIRADI KUELEKEA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

    May 06, 2025
  • MEI MOSI YALETA FARAJA KWA MAAFISA TARAFA GEITA.

    May 02, 2025
  • RC SHIGELA AIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WATUMISHI MKOANI GEITA.

    May 02, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAMPONGEZA MKURUGENZI MTENDAJI KWA KUPATA HATI SAFI

    April 30, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa