Jumla ya vyandarua 539,210 vyenye viuatilifu vya muda mrefu vinatarajiwa kugawiwa kwenye kaya zote katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ili kuhakikisha maambukizi ya Malaria yanapungua kwenye Mkoa wa Geita ambao kitaifa unashika nafasi ya tano katika maambukizi ya Malaria.
Hayo yamelezwa Agosti 1, 2024 katika semina ya uhamasishaji wa viongozi na mafunzo kwa watendaji ngazi ya mkoa na Halmashauri juu ya kampeni ya ugawaji wa vyandarua kwenye jamii (kaya) Mkoa wa Geita iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambayo imeratibiwa na Wizara ya Afya na OR-TAMISEMI ikishirikiana na Johns Hopkins Center for Communication Programs (JHUCCP) kupitia mradi wa PMI Vector Control Activity chini ya ufadhili wa Mfuko wa Rais wa Marekani (USAID) wa kupambana na Malaria.
Maafisa Kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na Kaimu Katibu tawala Wilaya ya Geita Bi Janeth Mobe wakiwa na wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita waliposhiriki semina ya uhamasishaji wa viongozi na mafunzo kwa watendaji ngazi ya Halmashauri juu ya kampeni ya ugawaji wa vyandarua kwenye jamii (kaya) iliyofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambayo imeratibiwa na Wizara ya Afya na OR-TAMISEMI ikishirikiana na Johns Hopkins Center for Communication Programs (JHUCCP) kupitia mradi wa PMI Vector Control Activity chini ya ufadhili wa Mfuko wa Rais wa Marekani (USAID) wa kupambana na Malaria.
Kufuatia taarifa ya Malaria ya dunia ya mwaka 2023, imeonyesha kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wa malaria kutoka wagonjwa Milioni 244 mwaka 2021 hadi kufikia wagonjwa milioni 249 mwaka 2022 huku vifo vitokanavyo na Malaria vikipungua kutoka 610,000 hadi vifo 608,000 mwaka 2021 na 2022 na kueleza kuwa kati ya wagonjwa wote asilimia 93.6 ya vifo vimetokea barani Afrika huku ikikadiriwa kuwa asilimia 93 ya Watanzania wanaishi katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa Malaria. Katika kutekeleza azma ya kupambana na ugonjwa wa Malaria kampeni ya TMC (Targeted Mass Campaign) imelenga kutekeleza majukumu tofauti tofauti ikiwemo uhamasishaji wa viongozi ngazi ya Mkoa na Halmashauri kusajili kaya kwa mfumo wa ki-elektroniki kwa ajili ya kupatiwa vyandarua, ugawaji wa vyandarua vilivyoainishwa kwa watendaji wa vijiji au mitaa pamoja na uhamasishaji juu ya matumizi sahihi na utunzaji wa vyandarua.
Washiriki wakifuatilia semina juu ya kampeni ya ugawaji wa vyandarua vyenye viutilifu kwenye jamii (kaya) katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ambapo jumla ya vyandarua 539,210 vyenye viuatilifu vya muda mrefu vinatarajiwa kugawiwa bila malipo kwenye kaya zote katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Akitoa semina hiyo Afisa Uhamasishaji Ndg Didas Misana kutoka Wizara ya Afya kitengo cha Kupambana na Ugonjwa wa Malaria amesisitiza elimu itolewee kwa jamii kuepukana na imani potofu juu ya vyandarua vinavyotolewa na kuvitumia kujikinga na mbu waenezao Malaria bila kuwa na wasiwasi wowote.
Pamoja na hayo jamii na viongozi wa dini wameaswa kuendelea kuihamasisha jamii juu ya zoezi la ugawaji wa vyandarua katika kaya zao na kuhimiza matumizi sahihi ya vyandarua sambamba na kutoa hamasa juu ya matumizi ya vyandarua na kutokomeza mila potofu juu ya matumizi ya vyandarua kwenye jamii ili kuendelea kuongeza umiliki wa vyandarua kwenye kaya na kufikia lengo la Shirika la Afya Duniani (WHO) la umiliki wa >80% (Chandarua kimoja kwa watu wawili)
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa