WAJUMBE wa Kamati ya Siasa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Geita wametembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya Shilingi Bilioni 9,244,350,934 inayo tekelezwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Akiongoza Kamati hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Geita Komredi Barnabas Mapande amesema Serikali inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa awamu ya sita inaleta fedha nyingi kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na kuwataka wananchi kuendelea Kumuombea Mhe Rais kwa kazi kubwa anayoifanya.
“Serikali ya awamu ya sita inaleta fedha nyingi za Miradi katika maeneo yetu kwa ajili ya kuwahudumia Wananchi hivyo nitoe rai kwa Wananchi kuilinda Miradi inayotekelezwa katika maeneo yao." Amesema Komredi Barnabas.
Katika upande mwingine Kamati hiyo imepongeza hatua ya Diwani wa Kata ya Kakubilo, Mhe Kesi Gayo Nyanda, kwa kutoa eneo lake lenye hekari sita kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Ikigijo, iliyopo katika Kijiji cha Kikwete, Kata ya Kakubilo yenye thamani ya Shilingi
Mapande amesema hatua hiyo ya Mhe Diwani kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule ni ya kuigwa na viongozi wengine katika kuchangia maendeleo.
Pamoja na pongezi hizo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita, Barnabas Mapande, amesema ili dhamira ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kufanikisha miradi kwa wananchi inatimia Serikali haina budi kuhakikisha mafundi wanaosimamia miradi wanakuwa na vigezo stahiki.
Ziara hiyo iliyo fanyika kwa siku mbili Januari 9 na 10, 2025 imetembelea Miradi ya Afya, Elimu, Maji na miundombinu ya Barabara ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
Kamati ya Siasa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Geita imetembelea Ujenzi wa Nyumba ya Mtumishi Kituo cha afya Busanda wenye thamani ya Shilingi Milioni 114,946,545.00. Ujenzi wa nyumba hiyo umetekelezwa na kujengwa na Mkandarasi DELTA MULTIHOLDINGS SOLUTION LTD na kusimamiwa kwa ushirikiano kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita na Mgodi wa Buckreef
Ujenzi wa Shule mpya ya Msingi Bwawani kupitia mradi wa BOOST wenye thamani ya Shilingi Milioni 348,500,000.Shule hiyo inaenda kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea umbali mrefu. Kamati ya Siasa imeipongeza Halmashauri kwa ujenzi wa shule hiyo katika kukabiliana na adha walizokuwa wakipata wanafunzi kutembea umbali mrefu.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani Geita Komredi Barnabas Mapande akimtua mama ndoo ya maji ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi katika Mradi wa Maji wa Katoro-Buseresere wenye thamani ya Shilingi Milioni 6,617,314,331 wenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita za ujao 2,500,000 kwa siku na kuhudumia zaidi ya wakazi 120,000 kwa kata za Ludete, Nyamigota, Katoro na Buseresere.
Kamati ya Siasa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ikikagua ujenzi wa Shule Mpya ya Ufundi ya Amali Kata ya Nyamigota kijiji cha Chibingo yenye thamani ya Shilingi Milioni 584,280,029. Kamati hiyo imeitaka Halmashauri kuwanyima kazi mafundi janja janja wanaochelewesha kazi ili wasiharibu kazi na kupoteza dhamira ya Mhe Rais kuwaletea wananchi maendeleo.
Ujenzi wa mradi wa shule mpya ya Sekondari Kakubilo kijiji cha Kikwete wenye thamani ya Shilingi Milioni 584,280,029 ambapo unatarajiwa kupunguza kwa kiwango kikubwa msongamano wa wanafunzi katika shule ya Sekondari Kakubilo
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa