Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba leo Februari 28,2025 ametembelea na kukagua ujenzi wa shule mbili za amali katika Jimbo la Geita na Busanda Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Akizungumza katika ukaguzi wa Miradi hiyo Mikubwa katika sekta ya Elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Mhe Komba amesema shule hizo zinaenda kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu ndani ya Wilaya ya Geita.
"Tunakila sababu ya kumshukuru Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha nyingi katika miradi ya shule hizi za amali Sekondari ya Nzera kiasi cha Shilingi Milioni 584.2 na Shule ya Sekondari ya Amali ya Chibingo kata ya Nyamigota kiasi cha Shilingi Milioni 584.2" Amesema Mh Komba.
Aidha Mhe Komba amempongeza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Rajab Magaro kwa usimamizi mzuri wa miradi ambayo Serikali ya awamu ya sita inaleta fedha nyingi.
" Nimpongeze Mkurugenzi Mtendaji kwa Usimamizi mzuri wa miradi kwa namna ambayo anasimamia miradi hii pamoja na Halmashauri kuwa na jiografia kubwa" Ameongeza Mhe Komba.
Pamoja na hayo Mhe Komba amesema lengo la ziara hiyo ni kukagua ujenzi wa miradi hiyo ili kuendelea kuwa na miradi yenye ufanisi na kuwataka wahandisi kuendelea kuongeza ueledi katika usimamizi wa miradi kuanzia hatua za awali ili miradi hiyo iweze kuwa imara na kuilinda.
Vilevile Mh Komba ameitaka Halmashauri kuendelea kuzingatia taratibu za manunuzi kupitia mfumo wa NeSt katika ukamilishaji wa Miradi pamoja na kuwasimamia mafundi kuongeza kasi miradi hiyo ikamilike kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Ndg Karia Magaro amezitaka kamati za Ujenzi katika Miradi hiyo kuendelea Kushirikiana katika shughuli za ujenzi wa miradi hiyo ili wanafunzi watakapo anza kuyatumia majengo hayo waone mandhari nzuri.
Shule hizo kila moja ina jumla ya madarasa 8, ofisi 2, Maktaba 1, Jengo la TEHAMA 1, Jengo la Utawala 1, Maabara ya Bailojia na Kemia pamoja na nyumba ya mtumishi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa