Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Martine Shigela, amepongeza juhudi zinazotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita, kupitia kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita za kuinua sekta ya Elimu nchini.
Akizungumza wakati akikagua ujenzi wa Mradi wa Shule mpya ya Amali, Nzera siku ya Maadhimisho ya Miaka 61 ya Muungano, Mh. Shigela amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo utachangia katika kuinua sekta ya Elimu kwa kuwapatia wanafunzi ujuzi, nje ya masomo ya kawaida.
“Niwapongeze Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kupata maendeleo ya miradi mikubwa ndani ya kipindi hichi cha miaka 61 ya Muungano. Ni matumaini yangu shule hii ya Amali itawapa nafasi wanafunzi kuweza kupata ujuzi wa ziada amabao utawasaidia kuweza kujiajiri pindi watakapomaliza masomo yao.” Amesema Mh. Shigela.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa