Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Martine Shigela, amezisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita, itaendela na juhudi za kuhakiskisha Watumishi wanaboreshewa maslahi yao pamoja na kuwapa stahiki zao kwa kuwa inatambua na kuthamini mchango wao katika ujenzi wa taifa.
Akizungumza katika sherehe za Mei Mosi hapo jana zilizofanyika kimkoa katika Viwanja vya CCM Kalangalala, Mhe. Shigela amesema kuwa Serikali inatambua changamoto zinazowakabili Watumishi wa Umma na Sekta binafsi zikiwemo ucheleweshaji wa malipo ya stahiki za wafanyakazi, ugumu wa kupata pensheni kwa wastaafu kwa wakati, pamoja na ucheleweshwaji wa madeni ya malipo ya ziada ya saa za kazi (Overtime), na kwamba mpaka sasa serikali imeshatoa kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 kwaajili ya kulipa malimbikizo ya madeni yao.
Aidha, Mhe. Shigela pia alibainisha kuwa hadi sasa chink ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluh Hassan, zaidi ya wafanyakazi 15,931 mkoani Geita tayari wamepandishwa madaraja, jambo ambalo kwa muda mrefu limekuwa ni kilio kwa Watumishi wengi Serikalini.
Kwa upande mwingine, Mhe. Shigela amesema serikali ina wajibu wa kutengeneza mfumo unaofanya kazi kwa ufanisi ili kuhakikisha mstaafu hatokumbana na usumbufu wowote wa kupata pensheni. Amesisitiza kuwa, kucheleweshwa kwa mafao ya Mstaafu ni uonevu na uvunjifu wa heshima ya mtumishi aliyeitumikia nchi kwa uadilifu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa