WASIMAMIZI wa uchaguzi wametakiwa kuzingatia suala la nidamu kazini pindi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakapoanza mwishoni mwa mwezi Novemba.
Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo kwa Wasimamizi Wa Uchaguzi vijijini, kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi Ndg. Karia Magaro, Afisa Msimamizi Msaidizi ngazi ya Halmashauri, Bi. Sarah Yohana amewataka wasimamizi hao kuwa makini pamoja na kuwa na nidhamu, hivyo wafanye kazi kwa uweledi.
“Zoezi la uchaguzi huwa linahitaji umakini na hivyo mnapaswa kuwa na nidhamu muda wote wa kazi. Vile vile mnatakiwa kutambua kuwa nyie ni watumishi wa umma kwa kuwa mmeaminiwa, hivyo mnatakiwa kuwa na maadili muwapo kazini lakini pia kuzingatia muongozo wa uchaguzi na kutunza siri.” Amesema Bi. Sarah Yohana.
Wasimamizi wa Uchaguzi wametakiwa kuzingatia uweledi pamoja na nidhamu wawapo kazini.
Bi. Sarah ameongeza kuwa, Wasimamizi wa Uchaguz wanatakiwa kuwapo vituoni ambapo zoezi la Uandikishaji kwenye daftari la Wakazi la Mpiga Kura muda wote wa kazi huku pia haiba ya Utumishi wa umma ikiendana na mavazi.
Kwa upande mwingine, mtendaji wa Kata ya Bugulula, Bw. Juma Choma amewataka wasimamizi kutoa taarifa kwa usahihi sambamba na kuzingatia suala la muda.
“Tujitahidi tutoe taarifa kwa wakati na kwa usahihi huku tukizingatia muda wa kuanza na kumaliza kazi. Usahihi kwenye kuandika majina (Yote matatu) ya wapiga kura itasaidia kupunguza ukakasi wa kuwa na sintofahamu wakati wa zoezi la uchaguzi.” Amesema Bw. Choma.
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya vijiji wakijaza fomu za viapo Octoba 8,2024 kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.
Bw. Choma pia amewataka Wasimamizi kuyatambua maeneo yao ya kazi mapema pamoja na kutengeneza mashirikiano na watendaji wa kijiji.
Aidha, Bw. Alphonce Sulwa, Mtendaji wa kata ya Kagu, ameongezea kwa kuwataka wasimamizi hao kufanya kazi kwa kuzingatia utu pamoja na kutokuwabagua mawakala wa uchaguzi kutokana na itikadi zao za vyama.
Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika nchini Novemba 27, mwaka huu.
Wasimamizi wa Uchaguzi wametakiwa kuzingatia muongozo katika kazi yao ikiwemo kutoka kwa viongozi wa vyama vya siasa kwa kuwa Watiifu, Waaminifu na kutunza siri.
Mambo Muhimu ya Kuzingatia:
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa