Na Hendrick Msangi.
Juhudi za Wananchi wa Mtaa wa Afya Kata ya Ludete iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Geita za kujenga maboma ya Shule ya Msingi zimeonekena baada ya Mkuu wa Wilaya ya Geita ndg Cornel Magembe kufanya Mkutano katika kitongoji hicho na kukabidhi jumla ya mifuko ya Saruji 210, Mabati 264 na Kiasi cha fedha shilingi Milioni moja na laki tano zilizopatikana kupitia wadau mbalimbali Mkoani Geita katika Kuunga Juhudi za Wananchi hao katika kukamilisha ujenzi huo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Geita Komredi Michael Msuya akiongea na Wananchi wa Kata ya Ludete mtaa wa Afya katika Mkutano wa Hadhara ambapo alisema Chama Cha Mapinduzi Kinaendelea kutekeleza Ilani yake ya Kushirikiana na Wadau mbalimbali Kuhakikisha changamoto za Wananchi zinatatuliwa.
Akizungumza Katika Mkutano Mkubwa uliofanyika katika viwanja vilivyo vilivyopo Kata ya Ludete ambapo Shule hiyo inajengwa, na kuhudhuriwa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Geita, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, wadau mbalimbali wa Maendeleo,Magembe amepongeza Juhudi za Wananchi hao kujenga shule hiyo yenye jumla ya madara sita na matundu nane ya vyoo.
Mamia ya Wananchi wa Kata ya Ludete wakiwa na furaha mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Geita baada ya matunda ya Juhudi zao za Ukamilishwaji wa Madarasa sita kuungwa Mkono na DC Magembe.
Ujenzi wa Shule hiyo ulifikiwa maamuzi ya kujengwa na wakazi wa Mtaa huo wa Afya kufuatia kutokea kwa matukio ya ajali zinazowakumba watoto wa shule wanaovuka ng'ambo ya barabara kufuata shule zilizopo maeneo mengine katika kata hiyo.
Katika Mkutano huo, Mkuu huyo wa Wilaya aliiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Geita kusimamia ukamilishwaji wa shule hiyo kwa hatua zitakazobaki ikiwa ni pamoja na Kuandaa Walimu kwa ajili ya Kufundisha watoto kuanzia ngazi ya elimu ya chekechea punde shule itakapokamilika ndani ya miezi miwili.
Maboma ya Madarasa ambayo yametokana na nguvu za Wananchi , ambapo yanatarajiwa kukamilika baada ya Juhudi zao kuungwa Mkono na Serikali kupitia Mkuu wa Wilaya ya Geita ndg Cornel Magembe.
Pamoja na hayo Magembe aliwataka Wananchi hao kuendelea kuziunga Juhudi za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea Wananchi Maendeleo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa