Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo John Dugange Disemba 18, 2021 amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa hatua waliyofikia katika ujenzi wa vyumba 352 vya madarasa baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule za Sekondari Lwezera, Bugando, Kagu, na Lutozo
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo Dkt.Dugange amesema kuwa Miradi hiyo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa imetolewa na Rais Samia kwa lengo la kuwasaidia watoto wa kitanzania kupata elimu bora katika mazingira bora ya kujifunzia sambamba na walimu ambao watafanya kazi katika Mazingira vutivu.
Aidha waziri Dkt.Dugange ametoa wito wa kujenga Miradi hiyo kwa kuzingatia thamani halisi ya pesa, ubora wa Miradi husika, sanjari na kuzingatia muda uliopangwa wa kumaliza ujenzi wa Miradi hiyo.
Awali akitoa taarifa kwa naibu Waziri huyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Paul Wanga alisema kuwa Miradi ya vyumba 350 kati ya 352 iko katika hatua ya umaliziaji huku madarasa mawili yaliyobaki yakiendelea kujengwa kwa kasi.
Aidha ameendelea kueleza kuwa katika kuhakikisha ujenzi huo wa vyumba 352 vya madarasa unakamilika kwa wakati Halmashauri ya Wilaya ya Geita iliajiri wahandisi wa nane kwa ajili ya kusimamia na kuongeza kasi ya ujenzi wa Miradi hiyo suala lililofanikisha hatua hiyo ya Miradi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa