Na Hendrick Msangi
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita Ndugu Nicolaus Kasendamila ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri.
Pongezi hizo zimejiri baada ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Geita ilipofanya ziara yake Februari 23, 2024 kwa kutembelea mradi wa shule ya msingi Nyaluhama iliyopo kata ya Bugalama Tarafa ya Kasamwa yenye jumla ya wanafunzi 552 wavulana wakiwa 290 na wasichana 262.
Ujenzi wa shule ya Msingi Nyaluhama umegharimu jumla ya kiasi cha shilingi 540,300,000 kutoka serikali kuu-BOOST, mradi huo umekamilika kwa madarasa 2 ya shule ya awali, madarasa 14 ya shule ya msingi, jengo la utawala, vyoo matundu 24 na kichomea taka.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya Siasa ya Mkoa, ambaye ndio Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita Ndugu Nicolaus Kasendamila aliitaka Halmashauri ya Kijiji kutafuta eneo kwa ajili ya uwanja wa michezo kwani ni muhimu kwa shule hiyo ambayo imejengwa katika ubora wa hali ya juu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita Ndugu Nicolaus Kasendamila amewataka wananchi Wilayani Geita kuendelea kupendana kama ambavyo Mhe Rais anavyowapenda kwa kuwaletea maendeleo ya miradi mingi ya shule zenye ubora, vituo vya afya na zahanati na miundombinu mizuri ya barabara
Aidha Ndugu Kasendamila aliwataka watumishi kupendana kwa kuwa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawapenda ndio maana analeta maendeleo Wilayani Geita.
Mkuu wa Wilaya ya Geita ndugu Cornel L.B Magembe akizungumza na wanafunzi, walimu na wananchi wa kata ya Bugalama Tarafa ya Kasamwa ambapo amewasisitiza kuendelea kulipa kipaumbele swala la Lishe shuleni hapo ili wanafunze waweze kupata chakula wawapo shuleni
Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Martine Shigela alipongeza ukamilishwaji wa mradi huo wa shule ya Msingi Nyaluhama ambapo alisema dhamira ya Mhe Rais ni kuwaondolea wananchi adha kwa kuwapunguzia mzigo wananchi ndio maana analeta fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo.”Mmeonyesha uwezo mkubwa, mmetekeleza kwa vitendo ukamilishwaji wa shule ya msingi Nyaluhama” alisema Shigela.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Martine Shigela amesema dhamira ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwaondolea wananchi adha kwa kuwapungizia mzigo kwa kuendelea kuleta fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya Taifa
Mradi mwingine ambao kamati hiyo ya Siasa Mkoa iliweza kuitembelea ni ujenzi wa nyumba ya watumishi 2in1 katika shule ya sekondari Nzera yenye jumla ya wanafunzi 260 ikiwa wavulana ni 122 na wasichana 138 huku walimu walio ajiriwa na serikali wakiwa 10.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nzera iliyopo kata ya Nzera ambayo ndio makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakifurahia ziara ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Geita wakati wa kuangalia mradi wa Nyumba ya watumishi 2in1 iliyogharimu kiasi cha shilingi 100,000,000 kutoka serikali kuu kupitia mfuko wa SEQUIP
Mradi huo wa nyumba ya watumishi 2in1 umegharimu kiasi cha Shilingi 100,000,000 kutoka serikali kuu kupitia mfuko wa SEQUIP ambapo familia mbili zipo tayari kuingia kwenye nyumba hiyo ikiwa ni juhudi za serikali ya awamu ya sita kuwawezesha walimu kufanya kazi katika mazingira mazuri
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyaluhama iliyopo kata ya Bugalama wakiwa na furaha baada ya kutembelewa na Kamati ya Siasa Mkoa wa Geita ambapo wametakiwa kuweka bidii kwenye masomo
Wakihitimisha ziara hiyo, Mwenyekiti huyo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita alimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndugu Karia Rajabu Magaro na kusema ujio wake umeleta chachu ya kukamilika kwa miradi ya maendeleo inayondelea kutekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Kamati ya Siasa Mkoa wa Geita ilitembelea Jengo la ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Geita lilipo kata ya Nzera ambapo walipongeza watumishi chini ya Mkurugenzi Mtendaji kwa Kuhamia katika jengo hilo
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa