Kiasi cha shilingi milioni 27 kimetengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa mwaka wa fedha 2020/2021, kwa ajili ya ukarabati wa mwalo wa Nkome Mchangani,ikiwa ni hatua mojawapo ya kuboresha Sekta ya uvuvi.
Taarifa ya makabidhiano ya ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, iliyowasilishwa na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi.Edith Mpinzile imeeleza kuwa, Halmashauri ya Wilaya ya Geita inakusudia kuboresha mialo yote, ili kuwa na mazingira rafiki kwa biashara.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Shughuli za ukarabati bado zinaendelea ambapo hadi sasa ujenzi wa ukuta wa kuzuia maji umefikia asilimia 75%.
Miongoni mwa changamoto zinazoathiri maendeleo ya sekta ya uvuvi katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ni pamoja na ufinyu wa bajeti,upungufu wa maafisa uvuvi, na upungufu wa vitendea kazi kama vile boti za doria .
Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina eneo la uvuvi katika ziwa Viktoria lenye ukubwa wa Kilometa za mraba 1,050, lenye jumla ya mialo 36, yenye vikundi vya usimamizi wa Rasilimali ya Uvuvi (BMUs) 32,na mabwawa 6 ya kufugia samaki.
Aidha idadi ya wavuvi ni 4,549, ambapo wenye mitumbwi ni 1,516, nyavu za makila 29,482, ndoano za kulaza 160,254, ndoano za kulowa 700 na makokoro ya dagaa 374.
Shughuli hizo za uvuvi zinailetea Halmashauri mapato kupitia leseni za uvuvi, leseni za wavuvi, ushuru wa samaki, pamoja na leseni za kukusanyia na kuuzia samaki.
Mnamo Agosti 20 mwaka huu alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Watendaji wa Kata,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Paul Wanga, alitoa ushauri wa kufunga mizani katika maeneo yote ya shughuli za uvuvi, ili kupata mapato sahihi kuliko kutumia mbinu ya makadirio.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa