Na: Hendrick Msangi
Kufuatia upepo mkali na mvua kubwa zilizonyesha siku ya Ijumaa Octoba 27, 2023, zimesababisha uharibifu mkubwa kwa Shule ya Msingi Kageya iliyoko Kata ya Nyachiluluma Wilayani Geita.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndugu Karia Rajabu Magaro akiwa na wajumbe wengine wakiwepo walimu, Mhe Diwani , pamoja na Watalam kutoka Halmashauri walipotembelea Shule ya Msingi Kageye iliyoharibiwa kutokana na mvua kubwa na upepo mkali.
Akizungumza mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Lusato Mashauri, alisema majira ya saa nne asubuhi wanafunzi wakiwa darasani, mvua kubwa zilizo ambatana na upepo mkali ziliengua mapaa ya madarasa matatu pamoja na ofisi ya Mkuu wa shule.
Hata hivyo hakukuwa na madhara ya Kibinadamu yaliyojitokeza kutokana na mvua hizo zilzoambatana na upepo mkali kwani walimu walishirikiana kuwahamisha wanafunzi hao na kuwapeleka kwenye madarasa mengine.
Mvua kubwa na upepo mkali vyaharibu madara ya shule ya Msingi Kageye Wilani Geita.
Naye Diwani wa Kata ya Nyachiluluma Mhe Rosa Musa alimuomba Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Karia Rajabu Magaro kuipa kipaumbele shule hiyo zinapokuja fedha za miradi." Tunaiomba Halmashauri kuzipa kipaumbele shule zilizo pembezoni kama shule hii ya Kageye" alisema Mhe Rosa.
Akikagua Uharibifu huo, Ndugu Karia Rajabu Magaro ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita alisema swala hilo linafanyiwa kazi kwa uharaka na kumtaka Diwani huyo kuendelea kuwahamasisha wananchi wa Kata hiyo kwa kujitoa kwa ajili ya shule hiyo wakati Serikali inaendelea kufanya taratibu za ukarabati wa madarasa yaliyoharibiwa.
Aidha Mkurugenzi alimuagiza Mhandisi wa Halmashauri hiyo kufanya ukarabati wa shule hiyo kwa uharaka ili wanafunzi hao ambao kwa sasa wanasoma kwa vipindi tofauti waweze kurejea katika utaratibu wao wa kawaida.
Shule ya Msingi Kageye iliyopo Kijiji cha Kageye kata ya Nyachiluluma Wilayani Geita ni shule kongwe iliyo anzishwa mwaka 1978 na kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 883 na Jumla ya Walimu 10. Kufuatia uharibifu huo shule hiyo imebaki na madarasa matatu huku madarasa matatu pamoja na Ofisi ya Mkuu wa shule kuharibiwa na mvua hizo.
Serikali inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutenga fedha nyingi kwa ajili Miradi ya shule katika halmashauri ya Wilaya ya Geita na tayari shule hiyo imetengewa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 37 kwa ajili ya kupaua na kukamilisha vyumba vitatu vya madarasa kutoka mfuko wa CSR.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa