Halmashauri ya wilaya Geita imetumia zaidi ya shilingi milioni 150 katika ujenzi wa mnada wa kisasa wa mifugo ulioko mji mdogo wa Katoro.
Hayo yamebainishwa na Afisa Utumishi wa halmashauri hiyo Donald Nsoko wakati akisoma taarifa ya ujenzi wa mnada huo ulipofikia kwa niaba ya mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, mbele ya mkuu wa mkoa Geita Mhandisi Robert Gabriel.
Amesema kuwa fedha zinazotumika katika ujenzi wa mnada huo zinatokana na fedha za uwajibikaji kwa jamii (CSR) zinazotolewa na kampuni ya Geita Gold Mining Limited GGML pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya Geita.
Katika mnada huo uliozingatia mahitaji yote muhimu ,Nsoko amesema mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi Milioni 365 hadi kukamilika kwake hali itakayo ongeza fursa ya kipato kwa Halmashauri.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel pamoja na kuipongeza halmashauri ya wilaya Geita kwa utekelezaji wa mradi huo, huku akishauri kuwekwa kwa nishati ya umeme katika eneo hilo.
Nao wananchi wa mji huo wa katoro wa wameshukuru kwa ujenzi wa mradi huo, na kusema kuwa hawatapata tena shida ya kupotelewa na mifugo yao mnadani.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa