Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Hashim Abdallah Komba, Julai 22, 2024 amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo tarafa ya Bugando kata ya Bugulula jimbo la Geita vijijini.
Akiwa kata ya Bugulula, Mhe. Komba ametembelea mradi wa shule shikizi ya msingi Kigoma iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi na kufikia hatua ya maboma yenye thamani ya shilingi milioni 58,510,000 mapato yaliyotokana na makato ya asilimia 20 kutokana na polisi jamii wanaolinda eneo la leseni ya uchimbaji ya mgodi wa dhahabu Geita (GGML) ambapo kijiji cha Bugulula hupokea shilingi 36,800,000.
Awali akimkaribisha kwenye kata hiyo, Diwani wa kata ya Bugulula Mhe.Lupuga Elisha amemuomba Mkuu wa wilaya kuwaunga mkono juhudi za kuanzisha ujenzi wa shule ya msingi shikizi Kigoma kwa kukamilisha vyumba 8 vya madarasa na ofisi 2 za walimu ili shule hiyo iweze kuanza kutumika ifakapo 2025.
Ujenzi wa shule shikizi ya Kigoma iliyo kata ya Bugulula ambayo imegharimu kiasi cha shilingi Milioni 58,510,000 nguvu za wananchi na mapato ya kijiji. Shule hiyo itaondoa changamoto ya mlundikano wa watoto katika shule mama ya msingi Bugulula pamoja na kupunguza umbali kwa watoto wa vitongoji viwili vya kigoma na migombani unaopeleka utoro na kukatiza masomo.
Kukamilika kwa shule hiyo kutaondoa changamoto ya mlundikano wa watoto katika shule mama ya msingi Bugulula ikiwa ni pamoja na kupunguza umbali kwa watoto wa vitongoji viwili vya kigoma na migombani unaopeleka utoro na kukatiza masomo.
Wananchi wa kata Bugulula wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba ambapo wamemuomba awasaidie kupata ardhi kwa wakala wa Huduma za misitu Tanzania ( TFS ) kwa ajili ya kilimo kufuatia ongezeko la mahitaji katika kata hiyo
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Rajab Magaro amesema Halmashauri kupitia mapitio ya bajeti itaangalia namna ya kuwezesha ukamilishwaji wa madarasa hayo.
Pamoja na kutembelea shule hiyo, Mhe. Komba ametembelea ujenzi wa ofisi ya kijiji cha Nyamilyango uliojengwa na wananchi kwa thamani ya shilingi milioni 8,359,000 ambapo ameiagiza ofisi ya Mkurugenzi kupitia idara ya Mipango , Maendeleo ya Jamaii na Utawala kuwasaidia wananchi kuibua miradi yenye kipaumbele.
Mradi wa ofisi ya kijiji cha Nyamilyango kata ya Bugulula kilichojengwa kwa nguvu za wananchi kwa thamani ya shilingi 8.3 ambapo ameiagiza ofisi ya Mkurugenzi kupitia idara ya Mipango , Maendeleo ya Jamaii na Utawala kutimiza wajibu katika kuwasaidia wananchi kuibua miradi yenye kipaumbele na kuwa na msukumo ili isikae muda mrefu bila kukamilishwa
Katika ziara hiyo, Mhe. Komba amefanya mkutano wa hadhara ambapo amewataka watumishi wa umma kusimamia fedha za serikali ili zifanye kazi iliyokusudiwa ili wananchi wapate huduma zinazostahili, ambapo serikali inatoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo. “Watendaji msome taarifa za mapato na matumizi, sitacheka na mtumishi wa umma yeyote atakayecheza na fedha za serikali”. Amesisitiza Mhe. Komba.
Kufuatia malalamiko ya wananchi juu ya uhaba wa ardhi ya kufanya kilimo, Mhe. Komba amewaagiza wakala wa Huduma za misitu Tanzania ( TFS )kuwaelimisha wananchi juu ya matumizi ya ardhi ambayo ipo kwenye hifadhi na sio kuwaacha kulima na kisha kuja kukata mazao yao na kuwataka kuwasaidia wananchi ili wapate maeneo katika utaratibu unaohitajika.” Nitoe rai kwa wananchi asiwepo mtu atakeyafanya kitu kinyume na taratibu za serikali” amesema Mhe. Komba.
Kuhusu swala la mikopo kausha damu ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa wananchi, Mhe. Komba ameiagiza Idara Maendeleo ya Jamii ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita kutoa elimu kwa wananchi juu ya mikopo inayotolewa na serikali ili wanufaike nayo na kuwataka wananchi kujitokeza ili wanaufaike na mikopo hiyo isiyokuwa na riba.
Akijibu kero ya mifugo kuharibu mazao , Mhe. Komba ameugaiza uongozi wa kijiji kuweka sheria zitakazo epusha migogoro ya wakulima na wafugaji na kuwataka wafugaji kuwaheshimu wakulima ili kuendelea kudumisha amani na utulivu.
Pamoja na hayo, Mhe. Komba amewasihi wananchi wa kata ya Bugulula kujitokeza kwenye uboreshaji wa daftari la mpiga kura ili kuboresha taarifa zao na kuwata viongozi wa chama na serikali kuendelea kuwahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa daftari la mpiga kura.
Wananchi wa kata ya Bugulula wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa Mkuu wa Wilaya ya Geita ambapo wameaswa kujitokeza kwa wingi katika uboreshaji wa daftari la mpiga kura ili waweze kurekebisha taarifa zao
Akihitimisha ziara hiyo, Mhe. Mkuu wa Wilaya amekemea vikali tabia ya wananchi wanaodhuru watu wenye ulemavu wa ngozi na kuwataka kuunganisha nguvu kupambana na tabia hiyo kwa kuwafichua wanaohusika na vitendo hivyo vya kikatili.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa