Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh.Rosemary sitaki Senyamule,ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wawekezaji, katika kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Ameyasema hayo Agosti 25 akiwa katika shule ya sekondari Evarist alipokuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita, ambapo amesema kuwa mahusiano mazuri kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita na wawekezaji, ndio yanayofanikisha kuendelea kwa miradi hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh.Rosemary Senyamule (katikati) baada ya kukagua baadhi ya majengo katika shule ya Sekondari Evarist kutoka (kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Paul Wanga akifuatiwa na diwani wa kata ya Nyarugusu Mh.Swalehe Juma Msene,(kutoka kulia )Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mh.Hadija Said Joseph.
Pongezi hizo zimekuja mara baada ya Mh.Senyamule kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari Evarist, iliyojengwa na mwekezaji ambaye ni mchimbaji wa madini ya dhahabu katika kata ya Nyarugusu Bw.Evarist Paschal,kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupitia mapato ya ndani,mradi wa CSR,nguvu za wananchi na mfuko wa jimbo.
Baadhi ya majengo mapya ya vyumba vya madarasa yaliyojengwa katika shule ya Sekondari Evarist.
Aidha amempongeza pia Bw.Evarist kwa mchango wake huo wa zaidi ya milioni 138, huku akitoa wito kwa wachimbaji na wadau wengine wa maendeleo, kuendelea kujitolea kusaidia katika miradi ya maendeleo kwa faida ya jamii.
Jengo la utawala katika shule ya Sekondari Evarist likiwa katika hatua za mwisho kuelekea kukamilika
Wakati huo huo Mh.Senyamule amewataka wanafunzi wa shule ya Sekondari Evarist ambao ndio wanufaika wa kwanza wa mradi huo, kuitunza miundo mbinu hiyo na kusoma kwa bidii, ili wapate matokeo mazuri, suala linalotazamiwa kama matokeo chanya ya miradi kama hiyo.
Ujenzi wa mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 251 umeanza April 2021, ikiwa ni mkakati wa kupunguza msongamano mkubwa wa wanafunzi katika shule ya sekondari Nyarugusu, ambapo mpaka sasa tayari vyumba sita vya madarasa na ofisi mbili zimekamilika.
Jiwe la msingi la shule ya Sekondari Evarist
Aidha jengo la utawala,vyoo vya walimu na wanafunzi,na maabara ,vyote viko katika hatua za mwisho za kukamilika, huku kisima kikiendelea kujengewa ambapo pia mabweni tu ndio bado hayajaanza kujengwa.
Mkuu wa Mkoa Wa Geita Mh.Rosemary Senyamule akisalimiana na baadhi ya wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita alipowasili katika shule ya Sekondari Evarist
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa