Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndg Karia Rajabu Magaro July 13 amefanya Ziara ya Kukagua miradi ya Maendeleo katika visiwa vya Izumacheli na Lulegeya vilivyopo ziwa Viktoria.
Akiwa Katika Ziara hiyo, Magaro amewataka wahandisi na mafundi ujenzi wanaotekeleza miradi ya maendeleo katika kata hiyo kushirikiana kwa Kufanya kazi kwa bidii na weledi huku wakizingatia taratibu za ujenzi kama zinavyoelekezwa na Serikali.
Ukarabati wa miundombinu ya Zahanati ya Izumacheli . Jumla ya kiasi cha Shilingi milioni 102 kimetengwa kukamilisha ukarabati wa choo, kichomea taka, nyumba ya mtumishi na jengo la OPD . Mradi huo unatarajiwa Kuhudumia zaidi ya watu 5000 katika kata ya Izumacheli.
" Mkawasimamie Wazabuni ili waweze kusambaza vifaa vinavyoendana na Miradi inayojengwa na sio kuchanganya vifaa na kuondoa ubora uliokusudiwa kwenye miradi" amesisitiza Magaro.
Pamoja na hayo Mkurugenzi Mtendaji Magaro amewataka wananchi kuendelea kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa miradi katika maeneo yao kwa kujitoa kwa nguvu zao na kukamilisha asilimia 10 wanayotakiwa kutoa katika miradi ya TASAF.
Ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa shule ya Msingi Lulegeya iliyopo kisiwani. Shule hiyo ina jumla ya Wanafunzi 125 na walimu 6. Mkurugenzi Mtendaji ameagiza Wahandisi kufanya makisio ya ukamilishwaji wa Madarasa hayo ili shule hiyo iwe na jumla ya vyumba 5 vya madara yanayotumika.
" Mnaposikia miradi ya maendeleo kupitia mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF mjitoe kwa nguvu zote na haraka kwa kuonyesha muitikio ili miradi ikamilishwe kwa wakati na kuanza kutumika ili kuendelea kuziunga juhudi za Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye analeta fedha nyingi za miradi ya maendeleo" amesema Magaro.
Aidha Mkurugenzi Magaro amemtaka Diwani wa Kata ya Izumacheli Mhe Cosmas Fidelis pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kuhamasisha wananchi ili waone umuhimu wa kuchangia asilimia 10 ya ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekezwa kupitia mfuko wa kunusuru kaya masikini (TASAF)
Mradi wa Kuchakata Samaki kata ya Izumacheli wenye thamani ya milioni 11 ambazo ni ufadhili kutoka Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) na Kanisa la AICT Geita. Mkurugenzi amewataka wanakindi hao kujipanga kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya jamii ili waweze kufaidia na Mikopo inayotolewa na Serikali ya awamu ya sita kupitia Halmashauri.
Ziara ya Mkurugenzi Mtendaji Ndg Karia Rajabu Magaro ni sehemu ya muendelezo wa ziara zake za kusimamia utekelezaji wa miradi inayotekezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Ukamilishwaji wa Mabweni ya Wanafunzi Shule ya Sekondari Izumacheli wenye thamani ya Shilingi milioni 200,900,000 kupitia mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF) ambapo asiliamia 10 ya nguvu za Wananchi ni shilingi Milioni 20. Mabweni hayo kila moja litabeba Wanafunzi 48
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaendelea kumshukuru Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi njema na nzuri anayoifanya ikiwa ni pamoja na kuleta fedha nyingi za miradi.
Jumla ya kiasi cha Shilingi Bilioni 2,130,560,056 zimepokelewa huku kiasi cha Shilingi Bilioni 1,168,560,058 zikiwa kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya mbili moja ikiwa ni ya Amali (shule ya ufundi)
Fedha nyingine kiasi cha Shilingi milioni 200,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili two in- one za watumishi katika shule mpya zilizojengwa mwaka 2023 za Nyakaduha na Kagega na kiasi cha Shilingi milioni 762,000,000 kwa ajili ya upanuzi wa miundombinu kidato cha tano na sita katika shule za Sekondari za Lutozo na Kagega.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa