Na: Hendrick Msangi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndugu Karia Rajabu Magaro, amezindua matokeo ya Upimaji ya mitihani ya Kitaifa katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita pamoja na kukabidhi tuzo na zawadi kwa shule zilizo fanya vizuri na zile zilizofanikiwa kuongeza ufaulu katika mitihani hiyo (PRE NECTA MKOA) kwa Mwaka 2022 kwa mitihani ya kidato cha pili (FTNA), kidato cha nne ( CSEE) na Kidato cha sita (ACSEE) kwa mwaka 2023.
Awali akitoa taarifa ya seksheni ya elimu sekondari kwa Mkurungezi katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri na kuhudhuriwa na wakuu wa shule za sekondari zilizopo katika Halmashauri hiyo, Kaimu Afisa Elimu Sekondari ndugu Richard Makoye alisema Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa sasa ina jumla ya Sekondari 75 ambapo 71 ni za serikali huku 4 zikiwa shule binafsi (Private schools)Aidha katika taarifa hiyo ilisema shule za serikali zina jumla ya wanafunzi 39,194 ambapo wavulana ni 20, 823 na wasichana idadi ikiwa ni 18,871, na kwa upande wa shule binafsi , wavulana ni 273 na wasichana ni 250 kufanya jumla ya wanafunzi 523 kwa shule binafsi.
Kwa upande wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ni 78, ambapo wasichana 34 huku wavulana wakiwa 44.
Pamoja na hayo Makoye alimueleza Mkurugenzi kuwa idara ya elimu inaishukuru Serikali kwa kutenga fedha nyingi kwa ajili ya Miradi ya ujenzi wa mindombinu ya shule za sekondari Butundwe ambayo ujenzi wa vyumba vya madarasa 8, mabweni mawili, matundu 13 ya vyoo ambapo gharama za fedha zilizo pelekwa kwa miundo mbinu hiyo ni kiasi cha shilingi 487,300,000Ujenzi mwingine ambapo fedha zimepelekwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya mtumishi 2 in 1 katika shule ya sekondari Nzera wenye thamani ya shilingi 100,000,000, nyumba ya mtumishi 2 in 1 shule ya sekondari Samia Suluhu wenye thamani ya shilingi 100,000,000, Madara 8 kwenye shule mpya kata ya Ludete wenye thamani ya shilingi 200,000,000, jengo la utawala, Tehama, Maktaba, Maabara(3) , matundu ya vyoo 8 wenye thamani ya shilingi 377,069,467, Ujenzi mwingine ni wa shule mpya kata ya Isulwabutundwe wenye thamani ya shilingi 577,069,467Akieleza hali ya ufaulu kwa Matokeo hayo Kaimu Afisa Elimu Sekondari ndugu Makoye alisema kiwango cha ufauli kwa mitihani ya Taifa kidato cha nne mwaka 2022 kimeongezeka toka asilimia 76.5 kwa mwaka 2021 na kufika asilimia 77.5 ambapo shule zilizofanya vizuri katika mitihani hiyo kwa mwaka 2022 ni pamoja na Shule ya sekondari Lutozo, Bugalama, Nkome huku shule zilizofanikiwa kuongeza ufaulu ni sekondari ya Nyaruyeye, Busanzu na BujulaAkiendelea kutoa taarifa hiyo kwa Mkurugenzi, Afisa elimu huyo alisema kwa upande wa mitihani ya upimaji wa kidato cha pili (FTNA) jumla ya Shule za sekondari 46 zilishiriki huku ufaulu ukiwa ni asilimia 86.7 ukishuka kwa asilimia 6.3 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka 2021 ambao ulikuwa asilimia 93.
Shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya upimaji wa kidato cha pili (FTNA) ni pamoja na Nyamalimbe, Magenge na Bugalama huku shule zilizofanikiwa kuongeza ufaulu katika mitihani hiyo ni shule ya Sekondari Lwemo, Nyamalinde na BusandaAkipokea taarifa hiyo, Magaro ambaye ni Mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Geita, aliwapongeza wakuu hao wa shule ambao shule zao zimeongeza kiwango cha ufaulu katika mithani hiyo.
“Natambua zipo shule bado hazifanyi vizuri ninawagiza sasa muongeze jitihada katika usimamizi wa shule zenu.
Tafiti mbalimbali zinaeleza wazi kuwa moja ya sababu za shule kufanya vizuri au vibaya ni aina ya uongozi uliopo katika shule husika” alisema Magaro.
Aidha aliwataka wakuu hao wa shule kuwa na ushirikiano katika utendaji wao na kuongeza juhudi katika utendaji ili kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeka huku akiwataka kuwa viongozi wazuri wakisimamia shughuli zote za kiuendaji katika shule zao ikiwa ni pamoja na miradi inayoendelea.
“Halmashauri itaendela kushirikiana na nyie kuwapa Motivation kwa walimu ambao wataleta matokeo mazuri katika shule zao” Alisema Mkurugenzi huyo.
Katika halfa hiyo, ndugu Magaro alitoa maelekezo kwa wakuu hao wa shule katika utendaji wa shughuli zao ambapo aliwataka kuhakikisha wanapokea na kutekeleza maelekezo ya Serikali ikiwemo uwasilishaji wa taarifa kwa wakati, kufuata sheria na miongozo na taratibu katika usimamizi wa shule.
Akiendelea kutoa maelekezo hayo, Magaro aliwataka wakuu hao wa shule kuisimamia miradi inayotekelezwa katika shule zao huku wakihakikisha majengo na mali za shule zinatunzwa vizuri.
Pia aliwataka wawe na mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka katika utendaji kazi wao pamoja na kuwa walezi na washauri wazuri kwa wanafunzi wanao wasimamia na kuwataka kuhakikisha mwaka ujao wa masomo ufaulu unaongezeka.
“Hakikisheni mnaanzisha masomo ya uchaguzi kwa wanafunzi kwa ajili ya kuwapanulia wigo wa ufaulu ikiwemo somo la Literature in English” alisema Magaro.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inamshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa shule za Sekondari .
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa