Katika Mkutano wake Maalum uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita-Nzera, Februari 7,2025, Baraza la Madiwani limempongeza Mkurugenzi Mtendaji Ndg Karia Rajab Magaro kufuatia mapendekezo ya kukusanya Kiasi cha Shilingi Bilioni 11.9 mapato ya ndani.
Akizungumza katika Baraza Hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazungu amesema Halmashauri imepata Mkurugenzi mtu bingwa na kupongeza uaandaji mzuri wa Bajeti hiyo ya 2025/2026.
"Kitu kikikosewa kwenye maandalizi lazima kilete mkanganyiko mkubwa sana. Nawapongeza sana ukiangalia bajeti tuliyo nayo ya Bilioni 8.3 na sasa tunaenda bajeti ya Shilingi Bilioni 11.9" Amesema Mhe Kazungu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Ndg Karia Magaro amelishukuru Baraza hilo pamoja na ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa Ushirikiano mzuri ambao umepelekea Halmashauri kufikia Bajeti hiyo.
Magaro ameongeza kwa kusema alipoingia Halmashauri alikuta Bajeti ya Halmashauri ni Kiasi cha Tsh Bilioni 5 baadaye Kiasi hicho kimeongezeka kwa kufika Bilioni 6 kwa mwaka wa fedha 2023/24 na mwaka wa fedha 2024/25 kufika Bilioni 8 na sasa kuelekea 2025/26 Halmashauri inatarajia kufikia Bilioni 11.9 mapato ya ndani.
"Nakupongeza Mwenyekiti wa Halmashauri na baraza lako kwa namna ambavyo tumefanya kazi kwa kushirikiana kupitia Wataalam, Watumishi kwani hii sio kazi ya mtu mmoja, Nilipokuja tulikuta Bajeti ya Bilioni 5 na baadaye ikaendelea kuongezeka kuwa Tsh Bilioni 6.4 tukavuka lengo na kwa mwaka wa fedha 2023-2024 bajeti ikawa Bilioni 7 na 2024 -2025 tukaenda Bilioni 8 na sasa kwa mwaka wa fedha 2025/2026 tunazungumzia bajeti ya Shilingi Bilioni 11.9." Ameongeza Ndg Magaro.
Aidha Ndg Magaro amewasihi Waheshimiwa Madiwani kuendelea kutoa ushirikiano kusimamia mapato ili adhma ya Halmashauri iweze kutimia kwa kuwa Bajeti hiyo imelenga kuwahudumia wananchi.
" Rais wetu anasisitiza tuweze kukusanya mapato ili Halmashauri ziweze kujitegemea kwa kiasi kikubwa" Amesema Ndg Magaro
Naye Katibu Tawala Wilaya ya Geita Bi Lucy Beda ametoa wito kwa Halmashauri kuendelea kuvisimamia vyanzo vya mapato vilivyopo ikiwa ni pamoja na Kuendelea kuongeza vyanzo vingine ili mapato yaendelee kuongezeka.
" Niipongeze Halmashauri kwani kwa Bajeti ya 2024/2025 malengo yalikuwa ni kukusanya Kiasi cha Shilingi Bilioni 8.3 na mpaka sasa kufika asilimia 58.3 hayo ni mafanikio makubwa ".Amesema Bi Lucy Beda
Aidha Bi Lucy Beda ametoa wito kwa Waheshimiwa Madiwani kuendelea kuisimamia vema Halmashaur ili malengo ya Bajeti hiyo yaweze kutimia kwa kuwa inaenda kuyagusa wananchi.
Baraza hilo limeidhinisha Rasimu ya mapendekezo ya bajeti Kiasi cha Shilingi Bilioni 93.5 kwa mwaka wa fedha 2025/2026 huku TARURA wakiwasilisha Mpango wa Bajeti kiasi cha Shilingi Bilioni 5.1, RUWASA Shilingi Bilioni 11.7 na kufanya Halmashauri kuwa na Rasimu ya mapendekezo ya bajeti kuwatumikia wananchi kiasi cha Shilingi Bilioni 110.4
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa