Wanafunzi wa shule ya Sekondari Buyagu wamefurahishwa na maendeleo ya Mradi wa vyumba sita vya madarasa unaoendelea katika shule yao.
Wakizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Paul Wanga Disemba 3, 2021 shuleni hapo wamesema kuwa kukamilika kwa Mradi huo kutawasaidia kusoma katika mazingira rafiki na vutivu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Wanga amewaasa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao kwa kuwa Serikali ya awamu ya tano inawajali na kuwaboreshea mazingira ya kujifunzia.
Wanga ametoa kauli hiyo alipotembelea shuleni hapo kukagua maendeleo ya Mradi wa ujenzi wa vyumba sita (6) vya madarasa vinavyojengwa katika shule hiyo kupitia fedha za mpango wa uviko 19 zilizotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Wanga amewaambia kuwa Rais Samia ameipatia shule hiyo ya Buyagu kiasi cha shilingi milioni mia moja ishirini (120,000,000) kwa ajili ya ujenzi wa vyumba sita vya madarasa ambayo yatakuwa na kiti na meza ili kuwarahisishia mazingira ya kujifunzia kwa lengo la kupata Elimu bora.
Ameendelea kusema kuwa jukumu walilonalo wanafunzi hao kwa sasa ni kusoma kwa bidii ili kufikia malengo yao huku akiwataka kuitunza miundombinu hiyo pindi itakapokamilika na kuanza kutumika.
Aidha Wanga amemshukuru pia Rais Samia kwa kuipatia Halmashauri ya Wilaya ya Geita shilingi bilioni 7 na milioni 940 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 352 na miradi kadhaa ya Afya inayoendelea kujengwa katika kata mbalimbali huku akifuatilia kila hatua ya maendeleo ya Miradi hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa