• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

TARURA YATAKIWA KUTEKELEZA MIUNDOMBINU YA BARABARA KABLA YA MSIMU WA MVUA KUANZA

Posted on: November 14th, 2024

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) Wilaya Geita wametakiwa Kutekeleza miradi ya miundombinu ya barabara zenye changamoto kabla ya msimu wa mvua kuanza pamoja na ujenzi wa madaraja ili kurahisisha Shughuli za maendeleo.

Hayo yamejiri Novemba 14,2024 Katika Kikao cha Baraza la Madiwani robo ya kwanza  kwa siku ya pili  katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri -Nzera ambapo Baraza hilo limepokea  taarifa za utekelezaji wa Shughuli za maendeleo ngazi ya Halmashauri kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba 2024.

Baraza hilo limepokea taarifa za Kamati za Kudumu za Halmashauri kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba ambapo Jumla ya kamati tano zimewasilisha taarifa zake.

Aidha kwa mujibu wa kanuni Na 22 ya kanuni za Halmashauri waheshimiwa Madiwani waliweza kuuliza maswali ya papo kwa papo na kupata majibu katika kamati hizo ambazo ni Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango, Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira, Kamati ya Elimu Afya na Maji, Kamati ya kudhibiti UKIMWI  na Kamati ya Maadili.

Katika Kikao hicho, waheshimiwa Madiwani wameiomba ofisi ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Wilayani Geita kutengeneza  miundombinu ya barabara zenye changamoto kabla ya msimu wa mvua.

Akizungumza katika Baraza hilo Mhandisi kutoka ofisi ya TARURA, Jerry Mwakapemba amelieleza Baraza hilo kuwa ofisi ya TARURA inaendelea Kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya barabara kulingana na bajeti zake kwa kila mwaka.


Mhandisi Jerry Mwakapemba kutoka TARURA akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miundombinu ya barabara katika baraza la madiwani 

Ofisi ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(TARURA) inahudumia mtandao wa Barabara za Vijijini (collector feeder and community roads) wenye jumla ya Kilometa 1745.79 zikiwepo barabara za lami km 4.2, changarawe km 655.07 na udongo km 1086.52 pamoja na madaraja 518.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauriya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazungu amewataka TARURA kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ili Barabara hizo zitoe huduma kwa Wananchi kuepusha madhara yanayoweza kutokea kutokana na ubovu wa miundombinu.

Kazungu ameongeza kwa kusema Halmashauri kupitia bajeti zake itatenga kiasi kwa ajili yakuiongezea nguvu TARURA ili kuendelea kukarabati miundombinu ya barabara kurahisisha shughuli za maendeleo.

Jumla ya Shilingi Bilioni 1.85 kutoka mfuko wa Barabara (road fund) imetengwa kwa ajili yakufanya ukarabati wa Barabara (maintenance) mfuko wa majimbo ya Geita na Busanda kiasi cha shilingi Bilioni 1 na Tozo ya mafuta kiasi cha Shilingi Bilioni 2.5.

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC KOMBA ARIDHISHWA NA UTEKEKEZAJI WA MIRADI KUELEKEA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

    May 06, 2025
  • MEI MOSI YALETA FARAJA KWA MAAFISA TARAFA GEITA.

    May 02, 2025
  • RC SHIGELA AIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WATUMISHI MKOANI GEITA.

    May 02, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAMPONGEZA MKURUGENZI MTENDAJI KWA KUPATA HATI SAFI

    April 30, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa