Na Hendrick Msangi
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi (CCM) na mwakilishi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Nadra Gulam Rashid, amefanya ziara Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Katika Ziara hiyo ya kukagua miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Geita, MNEC Nadra aliambatana na viongozi wengine wa chama na serikali
Ziara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo chini ya Serikali yao inayoongozwa na Mheshiwa Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MNEC huyo alipokea taarifa ya Ujenzi wa Miundombinu ya Afya Katika Hospitali ya Nzera, Ujenzi wa Hospitali hii umefanyika kupitia awamu tatu tofauti kulingana na Mapokezi ya fedha kutoka Serikali Kuu ambapo Jumla ya Tzs 2,806,000,000 zilipokelewa kutoka OR TAMISEMI kupitia fedha za bajeti ya Serikali mpango wa UVIKO 19 na SRWSS, ilisema taarifa hiyo ya Dkt Modest Buchard (MD.MPH) ambaye ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Geita
Aidha katika taarifa hiyo ya Utekelezaji wa Mradi huo, Dk Buchard alimueleza Mwenyekiti UWT , Ujenzi huo ambao umefanyika katika awamu tatu, umegharimu kiasi cha shilingi 1,500,000,000 kwa majengo saba ambayo ni Jengo La Utawala, Jengo la Wagonjwa wa Nje, Jengo la Maabara, Jengo la Ufuaji, Jengo la Mionzi, Wodi ya Wazazi na Jengo la Kuhifadhia dawa ambapo yote yamekamilika.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Dkt Modest Buchard akimtembeza MNEC Nadra Rashidi kukagua miradi ya maendeleo Hospitali ya Nzera.
Akiendelea katika taarifa hiyo, Dkt Buchard alisema awamu ya pili ilihusisha ujenzi wa wodi tatu za wanawake , wanaume na wodi ya watoto, ambapo Serikali kuu iliipatia Halmashauri kiasi cha shilingi 500,000,000 huku akitaja kutokamilika kwa ujenzi huo kutokana na kupungua kwa fedha zilizopokelewa.
Dkt Buchard alimueleza MNEC huyo, kuwa Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi 250,000,000 kupitia mpango wa UVIKO 19 kwa ajili ya awamu ya tatu ya ujenzi wa Jengo la wagonjwa mahututi(ICU) ambapo jengo hilo limeshakamilika na kuanza kutumika. Ujenzi mwingine uliokamilika katika awamu hiyo ni Ujenzi wa Kichomea taka cha kisasa (High Tech Incinerators), shimo la kutupia kondo la nyuma na shimo la majivu ambapo gharama za ujenzi zilikuwa jumla ya shilingi 56,000,000 ambazo zilipatikana kupitia progamu ya SRWSS.
Kupitia serikali Kuu inayoongozwa na Mh Dkt Samia Suluhu Hassan, hospitali hiyo imepokea vifaa tiba vya kisasa kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wanachi vikiwemo vifaa vya upasuaji, vifaa vya kujifungulia, vifaa kwa ajili ya wagonjwa mahututi pamoja na huduma ya vifaa vya mionzi (X Rays)
Akipokea taarifa hiyo, MNEC Nadra Gulam Rashid, alisema, Serikali inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga kuwafikia wananchi wote katika ngazi zote kuhakikisha huduma bora za afya, elimu , maji, miundombinu ya barabara na nishati ya umeme vinapatikana
MNEC Nadra Rashidi akipitia taarifa ya miradi iliyotekelezwa na Halmashauri ya Wilya ya Geita
Katika ziara hiyo ambayo baadaye ilifuatiwa na mkutano wa hadhara katika kata ya Nzera, Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Mh Joseph Musukuma, alimshukuru MNEC huyo ambaye alikuwa akimuwakilisha Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mama Mary Chatanda aliyekuwa kwenye kata nyingine za Halmashauri hiyo huku akimtaka amfikishie salaam za shukrani Mh Dkt Samia kwa kuwaletea maendeleo wana Geita-DC ambapo idadi ya Shule za Sekondari imeongezeka, uboreshaji wa huduma za afya na miundombinu ambapo wakandarasi wapo site kuendelea na kazi.
Aidha Mh Musukuma aliwasihi wananchi hao wa kata ya Nzera kuipa serikali yao muda na kuwahikikishia kupata huduma bora za kijamii likiwepo tatizo la umeme ambalo limekuwa ni kero kubwa.
Katika ziara hiyo iliyofanyika kwenye kata mbali mbali za Halmashauri ya Wilaya ya Geita, MNEC huyo pamoja na ujumbe wake waliweza pokea taarifa mbalimbali kutoka kwa wahusika waliopewa dhamana ya kusimamia miradi hiyo katika maeneo tofauti ya Halmashauri ya Geita DC.
Miradi mingine iliyotolewa taarifa kwa wajumbe hao waliofika kata tofauti za Halmashauri ya Geita DC ni pamoja na Ujenzi wa Miundombinu ya Kidato cha tano na sita shule ya Sekondari Butundwe yenye jumla ya wanafunzi 910 na walimu 22 ambapo ujenzi wake umefadhiliwa na Kampuni ya Barrick-Tanzania kwa gharama ya shilingi 487,300,000. Mradi huo haujakamilika kutokana na changamoto ya ucheleweshwaji wa malipo kwa mkandarasi.
Mradi wa ujenzi wa Bweni la Wasichana shule ya Sekondari Nyakagwe yenye jumla ya wanafunzi 175 ambao ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi 157,084,142.85 huku kiasi cha shilingi 17,550,000.00 sawa na asilimia 10 % ilichangiwa na wananchi na kiasi cha shilingi 139,534,142.85 sawa na asilimia 90% ilitolewa na mfuko wa maendeleo (TASAF). Mradi huu umekamilika kwa asilimia 100% ingawa bweni hilo halijaanza kutumika kutokana na changamoto za huduma ya umeme na maji.
MNEC Nadra alihitimisha ziara yake kwa kutembelea mradi wa kituo cha afya cha Kakubilo unaokadiriwa kuwa na gharama zinazofika kiasi cha shilingi 115,143,505 gharama hizo zikiwa ni nguvu ya wananchi, Halmashauri na CSR kupitia mgodi wa dhahabu Geita Gold Mine Limited (GGML).
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa