Huku ikiwa imesalia miezi michache nchi kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanashikamana na kudumisha tunu ya amani iliyopo, ambayo ndio msingi ulioasisiwa na Waanzilishi wa Muungano.
Akizungumza wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 61 ya Muungano wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kata ya Nkome, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mh. Martine Shigela amesema ya kuwa, Wananchi wanapaswa kuhakikisha kuwa wanazingatia suala la utulivu na kupendana pasi na kubaguana, haswa kipindi hichi ambacho nchi inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.
Mh. Shigela ameongeza pia kwa kuwataka Wananchi kuhakikisha wanajitokeza kujiorodhesha katika daftari la kupiga kura, zoezi ambalo linatarajiwa kuanza tarehe Mosi ya mwezi Mei, ili waweze kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba katika kuwachagua viongozi wanataoweza kuwawakilisha katika kuleta maendeleo kwenye maeneo yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa