MBUNGE wa Jimbo la Geita Vijijini Mhe Joseph Msukuma Julai 3, 2024, ameungana na waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Watumishi wa Halmashauri, Viongozi wa Chama na Serikali,ndugu jamaa na marafiki katika ibada ya Misa takatifu ya kuaga mwili wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Nyamboge Mhe Daud Simon Mlekwa aliyefariki June 30,2024 katika hospital ya Wilaya ya Geita -Nzera alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Mhe Joseph Kasheku Msukuma as amewaasa wanananchi wa Kata ya Nyamboge kutojihusisha na tabia za kuwakata mapanga watu wenye Ulemavu na kuwataka kuwafichua wale wote wanaojihusisha na tabia hizo. Msukuma pia ameeleza kusikitishwa kwake na msiba wa Diwani Daud Mlekwa na kuwaahidi Wananchi kuendeleza Miradi yote ambayo marehemu Mlekwa alikuwa akiisimamia katika kata hiyo.
Marehemu Mlekwa amekuwa Diwani wa Kata ya Nyamboge kwa kipindi cha miaka 9 toka mwaka 2015 kupitia chama Cha Mapinduzi (CCM) hadi umauti ulipomkuta akiwa bado ni Diwani wa Kata hiyo.
Wakizingumza kwa nyakati tofauti Viongozi wa Chama na Serikali wamemuelezea Diwani Mlekwa kuwa Kiongozi aliyewaunganisha Wananchi wa Kata ya Nyamboge kwa kushirikiana na wananchi na Halmashauri katika Kutekeleza Miradi ya Maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndg Salige Mkome amewaeleza mamia ya waombolezaji kuwa Halmashauri imepoteza Kiongozi aliyekuwa jemedari ,mwadilifu na mchapa kazi aliyeshirikiana na uongozi wa Halmashauri katika utekelezaji wa Shughuli za Maendeleo katika kata ya Nyamboge.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndg Salige Mkome amesema Marehemu Daud Mlekwa alikuwa Kiongozi jemedari mwadilifu na mchapa kazi katika kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo katika kata ya Nyamboge na kuongeza kuwa atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Naye Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita Cde Gabriel Nyasilu amesema kama chama kimepata maumivu kwa kumpoteza Kiongozi aliyewaunganisha wananchi na kutoa pole kwa Madiwani na uongozi wa Halmashauri kwa msiba huo mzito.
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita Komredi Gabriel Nyasilu amesema chama Cha Mapinduzi kimepata maumivu kwa kumpoteza Kiongozi aliyewaunganisha wananchi Katika kuleta Maendeleo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Hadija Said amesema marehemu Daud Mlekwa alikuwa kiungo kikubwa katika baraza la Madiwani katika utendaji kazi wake na kuwataka Wananchi wa Kata hiyo kuendelea kuyaenzi aliyokuwa akiyafanya na kuwahakikishia Miradi ya Maendeleo itaendelea Kutekelezwa na kuwataka wananchi kuwa watulivu.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Hadija Said amesema marehemu Daud Mlekwa alikuwa kiungo kikubwa katika baraza la Madiwani na kuwataka wananchi wa kata ya Nyamboge kuendeleza mazuri yote aliyoyaacha Marehemu Mlekwa.
Akizungumza katika Ibada ya Mazishi iliyofanyika Nyumbani kwa marehemu Mlekwa kijiji cha Chalameno kata ya Nyamboge Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini Mhe Joseph Kasheku Musukuma ametoa pole kwa Madiwani kwa kipindi kigumu walichopitia kwa kupoteza Madiwani wawili kwa kipindi kifupu ikiwepo kifo cha aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kamena Marehemu Peter Kulwa aliyefariki June 13, 2024.
Aidha amesema Serikali na chama vitaendelea Kutekeleza Miradi ya Maendeleo na kuwaahidi Wananchi wa Kata hiyo kuendelea kusimamia yale yote ambayo marehemu Mlekwa aliwaahidi wananchi wa Nyamboge.
Pia Mhe Msukuma ametumia nafasi hiyo kuwaasa Wananchi kuacha tabia za kukata mapanga watu wenye Ulemavu wa ngozi na kuwataka wananchi kuwafichua wale wote wenye tabia za kuwakata watu mapanga.
Marehemu Mlekwa ataendelea kukumbukwa kwa mchango wake mkubwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita katika kusimamia utekelezaji wa Shughuli za Maendeleo ndani ya Halmashauri.
Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakiwa katika hali ya huzuni na simanzi Katika Misa takatifu ya kuaga mwili wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Nyamboge Mhe Daud Mlekwa aliyefariki June 30,2024 katika hospital ya Wilaya ya Geita -Nzera alipokuwa akipatiwa matibabu.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa