Sherehe za Mei Mosi 2025 mkoani Geita, zimekua za kipekee baada ya Serikali kupitia kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuchangia zaidi ya Milioni 75 katika kusaidia kuondokana na changamoto ya uchakavu wa vyombo vya usafiri (Pikipiki) 20 kwa Maafisa Tarafa wote Mkoani Geita.
Akizungumza katika sherehe hizo zilizofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala, Katibu Tawala (M) Geita, Ndg. Mohamed Gombati amesema kuwa zoezi hilo la ugawaji wa vyombo hivyo vya usafiri limeleenga katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kuwawezesha Maafisa Tarafa kuwafikia kwa urahisi na kwa wakati wananchi katika maeneo yao.
Ugawaji wa pikipiki hizo ambazo zimegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 75,306,000 kutoka kwenye fedha za miradi ya maendeleo, ni sehemu ya Mkakati endelevu wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kuhakikisha inaboresha mazingira ya kazi kwa Watumishi wa Umma pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
Katika sherehe hizo, viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Wawakilishi wa Vyama vya Wafanyakazi walihudhuria, huku wakionyesha mshikamano, na kuthamini mchango wa Watumishi wa umma katika maendeleo ya taifa.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa