Maonesho ya saba ya madini yamekuwa na manufaa makubwa kwa wadau wa sekta ya madini, wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla hayo yamesemwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan katika Hafla ya kufunga rasmi maonesho ya saba ya Teknonojia ya madini Katika viwanja vya EPZ Bomba mbili Geita Mjini Oktoba 13, 2024. Maonesho hayo yaliyoanza oktoba 2,2024 na kumalizika tarehe Oktoba 13, 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza katika hafla ya kufunga maonesho ya saba ya madini
Maonesho haya yameleta manufaa kwa watu pia wasiojishughulisha na madini ikiwemo bodaboda, mamalishe na wafanyabiashara ndogondogo sasa jinsi tunavyoendelea maonesho haya si muda mrefu yanakwenda kuwa maonesho ya kimataifa aliongeza Mhe Rais.
Wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Geita ni mojawapo ya wanufaika wakubwa wa maonesho hayo.
Mamia ya wananchi wa mkoa wa Geita wakiwa katika viwanja vya EPZ Bomba mbili Geita Mjini katika hafla ya kufunga maonesho ya saba ya teknolojia ya madini
Sada H mganga ni mjasiriamali wa uuzaji wa dagaa wa Mwanza ambaye amenufaika na maonesho hayo, nimeyapenda, nimenufaika na uuzaji wa dagaa na kuona wateja wengi wakifika na kununua dagaa Katika banda hili natarajia maonesho mengine kuja na Dagaa wengi zaidi ili kuwafikia wateja wengi wanaofika katika maonesho hayo.
Merisiana Marendeja ni mjasiriamali wa Kuuza mvinyo wa Nanasi kutoka Igate, maonesho yaendelee tupate fursa ya kuuza zaidi bidhaa yetu na kuendelea kuitangaza zaidi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa