NZERA
Baraza la Madiwani halmshauri ya Geita wamekutana kwenye kikao cha robo ya tatu cha mwaka kujadili shughuli za maendeleo tarehe 29 April 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmshauri ya Geita.
Katika kikao hicho kikiongozwa na Mwenyekiti, Mhe Hadija Said amezungumzia changamoto mbalimbali ambazo zinatakiwa kutatuliwa kulingana na bajeti ya fedha 2024/2025 kama itakavyopangwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vyama vya Siasa (CCK) Ndg. Ramadhan Sengerema ameomba Halmashauri ya Wilaya Geita kutengeneza barabara za mtaani ambazo zimekuwa kero sana kwa baadhi ya wananchi pamoja na kuwasihi madiwani kufanya mikutano na wananchi wao.
Baraza hilo litaendelea Aprili 30,2025 kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo ngazi ya Halmashauri.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa