• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

MADIWANI HALMASHAURI YA GEITA WACHACHAMAA NA MPANGO WA CSR KUTOKA MGODI WA DHAHABU GEITA (GGML) KUTOKUKAMILISHA MIRADI

Posted on: November 12th, 2024

BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita Novemba 11, 2024 limekutana kujadili mapendekezo ya mpango wa wajibu wa kampuni ya Mgodi wa Dhahabu Geita (GGML) kwa jamii (CSR) 2024 katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.

Kikao hicho kilichowahusisha Kampuni ya Mgodi wa Dhahabu (GGML), Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita na Wataalam wa Halmashauri kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri -Nzera.

Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa miaka mitano imekuwa ikiingia makubaliano ya utekelezaji wa miradi na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML)  kupitia mpango wa wajibu wa mmliki wa Leseni  ya madini kwa jamii (CSR) ambapo kila mwaka Mkataba (MoU) wa Shilingi Bilioni 4,300,000,000 umekuwa ukisainiwa.

Utekelezaji wa wajibu wa kampuni kwa jamii (CSR) ni kwa mujibu wa kanuni kifungu Na 4-(1) cha mwongozo wa wajibu wa mmliki wa leseni wa mwaka 2023 ambapo kinamtaka mmliki wa leseni za madini kuandaa mpango madhubuti wa wajibu wake kwa jamii ambayo anaendesha Shughuli zake za uchimbaji wa Madini.

Awali Waheshimiwa Madiwani katika Baraza hilo wamehoji uongozi wa Mgodi wa dhahabu kutokukamilisha miradi ya maendeleo katika mpango  wa CSR wa mwaka 2021 hadi 2023 na kuagiza mpango huo utekelezwe ili wananchi waweze kunufaika na miradi ambayo  haijaanza kutumika kutokana na mpango huo kutokukamilika kwa wakati.

Ukamilishaji wa miradi ya mipango wa nyuma  umechukua muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali badhi zikiwa ni mchakato wa manunuzi unaofanywa na mgodi kuchukua muda mrefu, fedha za utekelezaji wa miradi hiyo kutokuwa halisi na gharama stahiki za miradi ikiwa ni pamoja na wazabuni waliopewa kazi na GGML kushindwa kupeleka  vifaa kwa gharama zilizoanishwa.

Katika baraza hilo, Mbunge wa Jimbo la Geita Mhe Dkt Joseph Kasheku Msukuma ameutaka uongozi wa Mgodi wa Dhahabu GGML kufuata taratibu kulingana na MoU wanazosaini ili kukamilisha miradi ya maendeleo.”Msiwe sababu ya kukwamisha miradi ya maendeleo kwa kutoa taarifa ambazo sio sahihi kwa viongozi wenu” Amesema Mhe Msukuma.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhe Mhandisi Tumaini Magesa ameutaka uongozi wa GGML kuvitambua vijiji ambavyo mgodi unaingia ili viweze kuingia kwenye mchakato vianze kupata stahiki zake kama vilivyo vijiji vingine ambavyo mgodi umefika.

Naye Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Geita Komredi Michael Msuya amewataka watumishi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) wanaosimamia miradi ya CSR kuwa wazalendo. “Muwe wazalendo kwenye hii nchi ili kuwasaidia wananchi wa Geita waweze kunufaika” amesema Cde Msuya.

Pamoja na hayo Cde Msuya amewaomba Wabunge waliohudhuria kikao hicho ambao ni Mhe Mhandisi Tumaini Magesa na Mhe Dkt Joseph Msukuma kuisaidia Halmashauri ili mifumo ya GGML ibadilike iwe na tija ili miradi viporo iweze kukamilika.

Akihitimisha kikao cha baraza hilo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazungu amewataka wataalam na waheshimiwa madiwani kila mmoja kutimiza wajibu  katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Vilevile Mhe Kazungu amewataka watumishi wa Mgodi wa Dhahabu GGML wanaosimamia miradi ya Maendeleo ndani ya Halmashauri kushughulikia swala la vijiji ambavyo vinapaswa kunufaika na CSR kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita  ili viweze kuingia kwenye mpango wa CSR

Baraza hilo limeridhia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa CSR 2024 kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita wa kiasi cha Shilingi Bilioni 4.3 ili utekelezaji wake uanze kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi inayoendelea kutekelezwa ili ianze kutoa huduma kwa Wananchi.

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC KOMBA ARIDHISHWA NA UTEKEKEZAJI WA MIRADI KUELEKEA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

    May 06, 2025
  • MEI MOSI YALETA FARAJA KWA MAAFISA TARAFA GEITA.

    May 02, 2025
  • RC SHIGELA AIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WATUMISHI MKOANI GEITA.

    May 02, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAMPONGEZA MKURUGENZI MTENDAJI KWA KUPATA HATI SAFI

    April 30, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa