• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

MADEREVA WA MAGARI YA SERIKALI WAPEWA MAFUNZO USALAMA BARABARANI-GEITA DC

Posted on: August 1st, 2024

Kampuni ya Uchimbaji madini ya Geita (GGML) kwa kushirikiana na Kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Geita Julai 31, 2024 imeendesha mafunzo ya usalama barabarani kwa Maafisa wasafirishaji na watumishi Halmashauri ya wilaya ya Geita yaliyoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita.

Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri yamelenga kuwakumbusha Maafisa wasafirishaji hao  sheria za usalama barabarani hususani katika barabara za kuingia katika mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) na uendeshaji unaozingatia sheria za usalama barabarani.

Meneja wa Idara ya ulinzi kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) ndg Sylvester Rugaba amewataka madereva wa serikali kuzingatia usalama wa barabarani na wanyamapori walipo ndani ya hifadhi ya mgodi kwani ulinzi wa wanyampori ni jukumu letu sote kuwatunza kwa kuendesha kwa kufuata alama za barabarani.

Akitoa elimu katika mafunzo hayo ya siku moja, Meneja wa Idara ya ulinzi kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) ndg Sylvester Rugaba amewaeleza Maafisa wasafirishaji hao kuwa ajali nyingi zimekuwa zikihusisha pia barabara za mgodini kutokana na uvunjaji wa sheria, hivyo utoaji wa mafunzo hayo unalenga hasa kuzuia ajali zisizo za lazima kwa kuhakikisha madereva wanazingatia sheria na taratibu za usalama barabarani.

Rugaba amesema kampuni ya uchimbaji wa madini Geita (GGML) imeamua kuendesha mafunzo kwa Maafisa wasafirishaji katika kuwakumbusha juu ya matumizi salama ya barabara kutumia njia za mgodini na nje ya mgodi ikiwa ni pamoja na ulinzi wa wanyamapori  waliopo kwenye hifadhi ya mgodi. “Ni jukumu letu sote kutunza wanyama katika hifadhi ya mgodi kwa kuendesha kwa kufuata alama za barabarani” amesema Rugaba.

Aidha Rugaba amewakumbusha madereva kuwa na vitambulisho na leseni pindi wanapoendesha magari  na kuwataka kusimama katika malango kwa  ajili ya ukaguzi , kuzingatia maagizo ya kiusalama  katika malango yote ya kuingia ili kuepuka matukio ambayo yanaweza kuleta  usumbufu kwa madereva pamoja na kutoa ushirikiano kwa kuwasiliana iwapo itatokea dharura.” Kuheshimiana,uadilifu kwa watoa huduma katika mageti ili kutunza usalama na kuacha kujihusisha  na vitendo viovu” amesema Rugaba. 

Sajenti wa jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Lucas Rwechungura amewaeleza  maderava wa serikali kutambua kuwa Familia zinawahitaji hivyo waongeze umakini kufuata sheria za barabarani huku wakiwa na akili timamu isiyokuwa na bugudha ili wanapoingia barabarani wawe na utulivu                                                                          

Naye Sajenti wa jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani Lucas Rwechungura amewataka madereva wa magari ya serikali kuzingatia matumizi sahihi na salama ya barabara ikiwa ni pamoja na kufuata sheria zote pindi wawapo barabarani.“Familia zinawahitaji hivyo ongezeni umakini kufuata sheria za barabarani huku mkiwa na akili timamu isiyokuwa na bugudha ili mnapoingia barabarani muwe na utulivu” amesisitiza sajenti Lucas.

Madereva wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakifuatilia mafunzo ya  usalama barabarani yaliyoratibiwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. Mafunzo hayo yameendeshwa na mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) kwa kushirikiana na Kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Geita.  

Kwa upande wake mwakilishi kutoka ofisi ya Katibu tawala mkoa, Ndg Geofrey Sweke amewaeleza madereva wa serikali kuzingatia sheria kwa kila wanachokifanya ili kuepuka vihatarishi huku akiwataka kutengeneza mbadala wa kutatua changamoto ambazo watakutana nazo na kusisitiza kufanya matukio yatakayo dhibiti vihatarishi.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya  Geita Dkt Modest Buchard ambaye ni mganga mkuu wa Halmashauri akifungua mafunzo hayo ya siku moja yaliyokuwa na lengo la kuwakumbusha madereva wa serikali  juu ya usalama  barabarani katika kutumia njia za mgodi wa dhahabu na nje ya mgodi ili kuepukana na ajali zinazoweza kuzuilika.  

Wakati huo huo Mwenyekiti wa madereva mkoa wa Geita Steven Kachungwa ameshukuru uongozi wa GGML, Mkoa pamoja na Halmashauri kwa ajili ya mafunzo hayo muhimu kwa madereva kuwataka  madereva kuendelea kuzingatia misingi ya maadili ambayo ni usalama, heshima, uadilifu, endelevu na ubora pamoja na kutunza vyombo vya usafiri wanavyovitumia.

Mwenyekiti wa madereva mkoa wa Geita Steven Kachungwa  amewasihi madereva kuendelea kuzingatia misingi ya maadili ambayo ni usalama, heshima, uadilifu, endelevu na ubora pamoja na kutunza vyombo vya usafiri wanavyovitumia.

Mwisho madereva walikula kiapo cha kuwa waaminifu katika kutii na kuziheshimu sheria za barabarani.

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC KOMBA ARIDHISHWA NA UTEKEKEZAJI WA MIRADI KUELEKEA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

    May 06, 2025
  • MEI MOSI YALETA FARAJA KWA MAAFISA TARAFA GEITA.

    May 02, 2025
  • RC SHIGELA AIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WATUMISHI MKOANI GEITA.

    May 02, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAMPONGEZA MKURUGENZI MTENDAJI KWA KUPATA HATI SAFI

    April 30, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa