KATIBU TAWALA Wilaya ya Geita Bi Lucy Beda, ameongoza mamia ya wananchi wa Geita kufanya usafi wa mazingira katika eneo la kituo cha mabasi Geita, Soko la Kariakoo Geita pamoja na upandaji wa Miti katika Shule ya Sekondari Kalangalala.
Hayo yamefanyika Leo Disemba 7, 2024 katika Halmashauri ya Mji wa Geita katika kuelekea maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Taifa la Tanzania ambapo Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita na Mji,Jeshi la Polisi, Jeshi la Akiba na Taasisi mbalimbali pamoja na wananchi wamejumuika katika zoezi la kufanya usafi pamoja na upandaji wa miti.
Katibu Tawala Wilaya ya Geita Bi. Lucy Beda akizungumza na wananchi katika Soko la Mbagala kuelekea maadhimisho ya siku ya uhuru
Akizungumza na wananchi mara baada ya zoezi la usafi na upandaji wa miti, lilioambata na michezo mbalimbali ya mbio za Mita 100, kukimbiza Kuku na kuvuta kamba, Bi Lucy ametoa rai kwa wananchi kuilinda amani ya nchi yao ili kuendelea kuwa na mshikamano.
Watumishi kutoka Halmashauri ya Wilaya na Mji Geita, vyombo vya ulinzi usalama, na wananchi wa Geita, wakifanya usafi wa mazingira.
“Tunafanya shughuli zetu kwa kuwa Taifa letu lina amani hivyo tuendelee kuenzi amani ya nchi yetu, kwani amani ikiondoka hatuwezi kufanya shughuli zozote” amesema Bi Lucy Beda.
Aidha Katibu Tawala huyo ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa wale wote ambao wana viashiria vya uvunjifu wa amani.
Mkoa wa Geita unatarajia kuadhimisha Siku ya Uhuru Disemba 9,2024 katika ukumbi wa GEDEKO –Geita Mji ambapo Mhe Martine Shigela Mkuu wa Mkoa wa Geita anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi.
Maadhimisho hayo yanabebwa na kauli mbiu isemayo “Miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara: “UONGOZI MADHUBUTI NA USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI NI MSINGI WA MAENDELEO YETU.”
Zoezi la upandaji miti katika mazingira ya shule ya sekondari Kalangalala na Michezo mbalimbali imefanyika ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya Uhuru
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa