Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita Agosti 6, 2024 limefanya Mkutano wake wa kawaida katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa lengo la kuwasilisha taarifa juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa ngazi ya kata katika robo ya nne Aprili hadi Juni 2024 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kwa kata zote 37 za Halmashauri.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe Charles Kazungu(kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji Ndg Karia Magaro wakati wa Kikao cha baraza la Madiwani
Akizungumza kwenye Baraza hilo Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Mhe. Charles Kazungu amewataka Watendaji wa vijiji kufafanua kwa undani zaidi juu ya miradi mipya ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa katika Kata zao na kueleza hatua gani miradi hiyo imefikia pamoja na kuzingatia namna nzuri ya uandikaji wa taarifa wanazowasilisha.
Cde Michael Msuya Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Geita amawasihi madiwani kuendelea kusimamia vema suala la ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Geita Cde Michael Msuya amelipongeza baraza la madiwani kwa namna ambavyo wanasimamia miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na watumishi wa halmashauri wanavyofanya kazi kwa weledi kuhakikisha dhamira ya Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwatumikia wananchi inatimia.
Waheshimiwa Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakiwa katika Kikao cha baraza la madiwani ukumbi wa Halmashauri ambapo wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa ngazi ya kata.
Pamoja na hayo Cde Msuya ameitaka Halmashauri kupitia idara ya Elimu kutumia mapato ya ndani ili kuendelea kuajiri walimu wa muda kwa masomo ya sayansi wakiwemo wa walimu wa kike wakati wakiendelea kusubiri serikali inapoendelea na mchakato wa kuongeza ikama ya walimu.
Vilevile, Cde Msuya amekemea tabia ya utoro wa watoto mashuleni unaopelekea kushuka kwa ufaulu na kuwataka watendaji kuendelea kusaidia kupunguza utoro mashuleni.
Mbali na hivyo Cde Msuya amawasihi madiwani kuendelea kusimamia vema suala la ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Ndg Karia Magaro amelieleza Baraza hilo kuwa Menejimenti itaendelea kufanya utekelezaji wa yote yaliyowasilishwa kwa ajili ya mustakabali wa Halmashauri.
Waheshimiwa Madiwani wakiwasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ngazi ya kata katika kikao cha baraza la madiwani Agosti 6,2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa