Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati, ametembelea timu za Halmashauri kutoka mkoa wa Geita zinazoshiriki mashindano ya Shimisemita 2025 yanayoendelea jijini Tanga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati (wa pili kushoto), akizungumza na viongozi wa Timu na wanamichezo wanaoshiriki mashindao ya Shimisemita Jijini Tanga.
Akizungumza na wachezaji na viongozi, Gombati amepongeza maandalizi mazuri aliyojionea akisema: “Nimefurahishwa na maandalizi niliyoyakuta, timu zetu zote zipo vizuri na wamenihakikishia wapo tayari kwa ajili ya ushindani.”
Aidha, ametoa shukrani kwa Rais kwa kuendelea kuhamasisha michezo na kujenga mazingira rafiki kwa watumishi kushiriki mashindano hayo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi kutoka Mkoa wa Geita wanaoshiriki mashindano ya michezo jijini Tanga.
Gombati amesisitiza kuwa michezo hii ni nyenzo muhimu ya kujenga ushirikiano, mshikamano na ushindani chanya katika serikali za mitaa, huku akiwataka wachezaji kudumisha nidhamu na kuhakikisha wanapata ushindi.
Vilevile, amepongeza wakurugenzi wa Halmashauri zote za Geita kwa maandalizi waliyoonyesha na kutumia nafasi hiyo kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa wa mwaka 2025 kwa amani na mshikamano.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mohamed Gombati, akikabidhi zawadi kama ishra ya motisha kwa wanamichezo wanaondelea na mashindano ya Shimisemita Jijini Tanga
Kwa upande wake, Afisa Michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Julius Laizer, alimshukuru Katibu Tawala huyo kwa hamasa aliyoitoa kwa wachezaji na kuwatia moyo kuelekea mashindano hayo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa