Kampuni ya dhahabu ya Buckreef yenye ubia na Shirika la madini la taifa STAMICO imetiliana saini mkataba wa shilingi milioni 321 na Halmashauri ya Wilaya ya Geita ili kuwekeza katika miradi ya Elimu na Afya.
Fedha hizo zimeelekezwa kutumika katika kata nne ambazo ni Busanda, Kaseme, Bugulula na Lwamgasa ikiwa ni mpango wa utekelezaji wa sheria ya uwajibikaji wa kampuni kwa jamii (CSR).
Akizungumza katika hafla hiyo mkuu wa mkoa wa Geita Rosemery Senyamule ameishukuru kampuni hiyo na kuahidi ushirikiano huku akiitaka Halmashauri ya Wilaya ya Geita kusimamia vyema matumizi ya fedha hizo ili zitumike kama ilivyokusudiwa na kuleta tija kwa wananchi.
Kwa upande wake kaimu meneja mkuu wa kampuni ya dhahabu ya Buckreef Isaac Bisansaba amesema kuwa fedha hizo ni uwajibikaji wa kampuni kabla ya uzalishaji na kwamba wamezielekeza fedha hizo katika sekta za elimu na afya kwa kuwa ni vipaumbele vya serikali.
Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la madiwani halmashauri ya Wilaya ya Geita Charles Kazungu mbali na kubainisha fedha hizo maeneo zitakapotumika ameipongeza kampuni ya Backreef kwa usikivu pale Halmashauri ya Wilaya ya Geita ilipotoa mapendekezo tofauti na mipango yao ya awali na wakakubali mapendekezo hayo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa