Kamati ya Uratibu wa Mwenge kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Geita, imeweza kupitia na kukagua miradi mbali mbali, pamoja na njia iliyopendekezwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kuwasili Mkoani Geita mnamo tarehe 1, Septemba mwaka huu, ambapo Halmashauri ya Wilaya, Geita itakua ya kwanza kuupokea ukitokea mkoani Mwanza.
Akizungumza tarehe 24, Juni wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndg. Deodatus Kayango ameiagiza Halmashauri ya Wilaya kuhakikisha kuwa maadalizi yanakuwa vizuri, miradi inaakisi thamani ya fedha, pamoja na kuziweka nyaraka zote muhimu za miradi ili Mkoa uweze kufanya vizuri.
Aidha, kamati hiyo pia imetoa mapendekezo kwa timu ya Wahandisi kuhakikisha wanaikagua miradi hiyo mara kwa mara ili kujiridhisha, kuzingatia huduma zote za msingi; Maji na Umeme zinapatikana kwenye miradi hiyo, pamoja na kuwakazania Wakandarasi waweze kuikamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Kwa upande wake, Mratibu wa Mwenge wa Uhuru kutoka Halmashauri, Ndg. Alexander Herman amesema kuwa Kamati ya Hamasa itahakikisha hamasa inatolewa kwa wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi kuupokea Mwenge huo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa