• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YAGEITA YAKAGUA NJIA YA MWENGE WA UHURU 2024

Posted on: September 10th, 2024

MWENGE wa Uhuru 2024 unatarajiwa kupokelewa  Mkoa wa Geita Septemba 30, 2024 na kukimbizwa katika Halmashauri 6 za Mkoa wa Geita ambazo ni Chato ( Septemba 30,) Bukombe (Octoba 1) Mbogwe (Octoba 2) Nyang’hwale (Octoba 3)Geita mji (Octoba 4) na Geita Dc (Octoba 5, 2024) huku ukibeba kauli mbiu isemayo “Tunza Mazingira na shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu.”

Katika kuendelea na maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru ifikapo Octoba 5, 2024, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilayani Geita ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba  Septemba 9 ,2024 imefanya ziara ya kukagua njia ya Mwenge wa Uhuru ili kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika mbio za Mwenge wa Uhuru ambao utapokelewa katika viwanja vya shule ya msingi Bugulula ukitokea Halmashauri ya Mji wa Geita.

Wananchi wakiwa katika eneo la mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya shule ya msingi Bugulula wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ilipofanya ziara ya kukagua njia ya Mwenge wa Uhuru 2024

Kamati hiyo imetembelea miradi yote itakayotembelewa na Mwenge wa Uhuru ambapo imeendelea kutoa Hamasa kwa wananchi wa maeneo yote kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru ambao utazindua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Geita ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe Hashim Abdallah Komba ikiwa katika ukaguzi wa Njia ya Mwenge wa Uhuru unaotarajiwa kupokelewa Octoba 5, 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa Octoba 5, 2024 kata ya Bugulula ambapo utakimbizwa sehemu mbalimbali ndani ya halmashauri na baadaye kukesha katika viwanja vya kituo cha mabasi kilichopo kata ya Nkome.

Wananchi wakiwa katika Kituo cha Afya Nkome wakati kamati ya Ulinzi na Usalama ilipotembelea miradi ya maendeleo itakayo zinduliwa na kufunguliwa na Mwenge wa Uhuru Octoba 5, 2024

Pamoja na hamasa iliyotolewa kwa wananchi kushiriki katika mbio hizo, pia kamati  ya ulinzi na usalama imetumia nafasi hiyo kuendelea kuwakumbusha wananchi kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Mbio za Mwenge wa Uhuru zinachochea na kuhamashisha tunu za taifa ambazo ni amani, uzalendo, umoja na mshikamano ndani ya Taifa na pia kuchochea shughuli za maendeleo.

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • WANANCHI WAHIMIZWA KULINDA AMANI NA UTULIVU KUELEKEA UCHAGUZI MKUU-CPA AMOS MAKALLA

    May 20, 2025
  • RUSHWA NI JANGA LINALOATHIRI MAENDELEO YA KIUCHUMI, KIJAMII NA KISIASA NCHINI-RAS GOMBATI.

    May 13, 2025
  • GEITA YAPATA MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI.

    May 12, 2025
  • ALAT MKOA WA GEITA WAMPONGEZA MKURUGENZI GEITA DC USIMAMIZI MZURI WA MIRADI

    May 10, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa