• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WILAYA YA GEITA YAWAFARIJI WAHANGA WA MOTO KATIKA SOKO LA CCM KAKUBILO

Posted on: January 28th, 2022

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe.Wilson Shimo ametoa wito wa kuwataka wanachi wanaofanya biashara katika masoko mbalimbali kuchukua tahadhari za kukabiliana na ajali za moto kwa kuboresha miundo mbinu na kutokutumia vyanzo hatarishi vya moto katika mazingira hayo.

Ameyasema hayo Januari 27 alipoambatana na kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Geita pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita wakati akizungumza na wafanyabiashara wa soko la CCM Kakubilo walipokwenda kuangalia athari za ajali ya moto uliotokea usiku wa Januari 25 na kuteketeza vibanda 16 vya biashara katika soko hilo.

Mhe.Shimo amesema kuwa ubora wa miundo mbinu katika masoko unaweza kusaidia kudhibiti athari zaidi pale ajali ya moto inapotokea kwa kuwa magari ya zimamoto yanaweza kufika na kuingia kona zote kwa urahisi huku akimtaka Mkuu wa jeshi la polisi Wilaya kuwatafuta watu waliohusika kuiba baadhi ya bidhaa za wafanyabiashara wakati wa ajali hiyo huku akikemea vikali tabia za kuiba mali za watu pindi yanapotokea majanga.

Naye Mkuu wa jeshi la zimamoto Wilaya ya Geita Inspekta Stanley Lwago amewataka wafanyabiashara hao kuendelea kuchukua tahadhari za moto kwa kutenganisha maeneo ya kufanyia biashara na shughuli za mapishi, kuwa na vifaa vya kuzimia moto, na hata kufunga vifaa maalumu vya kung’amua moto  majumbani na sehemu za biashara vinavyotoa taarifa ya moto ukiwa katika hatua ya chini kabisa baada ya kuhisi moshi, huku akishauri kupishanisha kuta zinazotenganisha vyumba ili kuzuia moto kuhamia chumba kingine kwa urahisi.

Awali mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Mhe.Charles Kazungu licha ya kutoa pole kwa wahanga hao amemuomba Mkuu wa Wilaya kusaidia kuangalia njia mbadala ya kuwezesha Halmashauri ya Wilaya ya Geita kupata angalau magari mawili ya zimamoto ya kuazia  hata kama ni kwa kupitia fedha za CSR ili kusaidia katika kukabiliana na majanga ya moto katika tarafa za Busanda na Bugando.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita John Paul Wanga awali akitoa taarifa kwa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya alisema kuwa tukio hilo lilitokea Januari 25 majira ya saa mbili kasorobo usiku huku akiwashukuru wananchi ambao walishiriki kuuzima moto huo ambao umeleta madhara ya kuunguza mali pekee bila madhara kwa binadamu.

                                              

Baadhi ya Wahanga wa ajali hiyo ya moto akiwemo Bw.Renatus Elias aliyekuwa na duka la nguo amesema kuwa ajali hiyo imeathiri mtaji wake kwa kuwa mali yenye thamani ya shilingi milioni 8 imeteketea kwa kuungua na baadhi ya mali kuibiwa na watu wasio na nia njema wakati alipokuwa akijaribu kuokoa mali zake usiku huo.

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC KOMBA ARIDHISHWA NA UTEKEKEZAJI WA MIRADI KUELEKEA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

    May 06, 2025
  • MEI MOSI YALETA FARAJA KWA MAAFISA TARAFA GEITA.

    May 02, 2025
  • RC SHIGELA AIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WATUMISHI MKOANI GEITA.

    May 02, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAMPONGEZA MKURUGENZI MTENDAJI KWA KUPATA HATI SAFI

    April 30, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa