Jamii imeendelea kukumbushwa kuhamasika kupanda Miti kwa wingi katika maeneo yao ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya Nchi suala linalosababisha ukosefu wa Mvua katika maeneo mbalimbali Nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mheshimiwa Wilson Shimo ametoa rai hiyo wakati akiongoza zoezi la kupanda miti katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Disemba Mosi 2021, zoezi lililofanyika katika uwanja wa Zahanati ya Nkome katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita .
Baada ya kupanda mti wake katika eneo hilo Mheshimiwa Shimo aliwataka viongozi mbalimbali kuikumbusha jamii utamaduni wa kupanda kwa wingi miti katika mazingira yetu na kuitunza ili kuirudisha dunia katika Uasili wake suala litakalotuepusha na majanga mbalimbali ikiwemo ukame.
Aidha katika kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani iliyofanyika ki Wilaya katika kata ya Nkome katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita viongozi mbalimbali walipanda miti ya kumbukumbu katika eneo hilo la Zahanati ya Nkome kama ishara ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa