Huduma ya afya ya Mama na mtoto pamoja na wajawazito imetajwa kuimarika ndani ya kituo cha afya katoro baada ya kukamilika kwa majengo na vifaa vya kusaidia wakina mama wakati wa kujifungua.
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya katoro daktari Manigina Philemon amesema huduma kwa wajawazito imekuwa bora ikilinganishwa na awali ambapo wajawazito wanne walilazimika kulala kitanda kimoja hali iliyokuwa inaongeza hofu ya kuwalinda watoto baada ya kuzaliwa.
Badhi ya wananchi wanaopatiwa huduma katika kituo hicho wamesema mabadiliko ya huduma yamepunguza gharama za kusafiri umbali mrefu kupata huduma wakati wa kujifungua
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Geita Barnabas Mapande anamini juhudi za kuboresha miundombinu ya afya itasaidia kupunguza vifo vya mama mjamzito na mtoto
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa