Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita Nzera,inategemewa kuanza kutoa huduma za kibingwa kila mwezi ifikapo septemba mwaka huu, kwa lengo la kuwasogezea huduma wagonjwa mbalimbali.
Hayo yamebainishwa leo agosti 24, na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Geita
Dkt.Modest Rwekaemula, ambapo amesema kuwa, huduma hizo zinatarajiwa kuanza kutolewa kufikia mwezi wa tisa mwaka huu,kwa kuwa kuna Madaktari wa kutosha,maabara,vifaa tiba na miundombinu mingine ya muhimu.
Majengo mawili ya wodi yanayoendelea kujengwa katika hospitali ya wilaya ya Geita Nzera
Ameelezea ujenzi unaoendelea hospitalini hapo wa majengo matatu ambayo ni wodi za wanawake,wanaume na watoto,kwamba umefikia 80% na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi septemba mwaka huu.
Amesema kuwa ujenzi wa wodi hizo umefanyika kupitia fedha zilizotolewa na Serikali kuu,kiasi cha shilingi milioni 500.
Akifafanua zaidi amesema kuwa awali Serikali kuu ilileta hospitalini hapo kiasi cha shilingi bilioni 1 na milioni 800 ambazo zilitumika kujenga majengo ya utawala,wagonjwa,maabara,jengo la ufuaji (laundry),jengo la mionzi,wodi ya wazazi na jengo la dawa ambayo kwa sasa yanatumika.
Jengo la wodi katika hospitali ya wilaya ya Geita Nzera
Aidha amewataka wananchi kuiamini Hospitali hiyo kwa kuwa imeboreshwa Zaidi kwa lengo kuwapatia huduma bora za afya.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa