Watoto walio na umri chini ya miaka mitano wapo katika hatari zaidi ya kukumbwa na magonjwa ya degedege, kupatwa na mtindio wa ubongo,matatizo ya moyo na kupata matezi, endapo hawatapata chanjo ya sindano za Surua-Rubella na Polio.
Katika kuadhimisha lengo la kampeni ya kitaifa ya kuzuia na kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo amabayo ni Surua,Rubella na Polio, Mganga Mkuuwa mkoa wa Geita Dokta Japhet Simeo amesema kuna hatari ya kuongezeka vifo kwa watoto walio na umri chini ya miaka 4 kama Wazazi hawata chukua jitihada mapema za kuwapeleka watoto wao kupata chanjo hizo
Uthibitisho wa kitalaamu unaonyesha kwamba ni asilimia 85 tu ya watoto wanapata kinga kamilifu ya chanjo ya surua wakati wanapotomiza miezi 9 huku wototo wengine asilimia 15 hawapati kabisa huduma za chanjo.
Kwa Upande wa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ambaye ameongoza uzinduzi wa kampeni hiyo kwa Mkoa wa Geita iliyozinduliwa katika hospital ya Halmashauri ya Wilaya Geita,Hospital ya Nzera amesema Lengo la Mkoa ni kupambana na magonjwa yanayozuilika na kuwachanja watoto wote waliolengwa
Mkoa wa Geita umelenga kuwachanja watoto 413,874 kwa chanjo ya Surua Rubella na watoto 171,325 kwa chanjo ya Polio ya sindano kwani Mkoa unakiwango cha kutosha cha Chanjo, na kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita huduma hii ya chanjo itatolewa katika vituo vyote vya afya na vituo vitakavyoelekezwa na Halmashauri.
Chanjo hizi zitatolewa kwa siku tano (5) kuanzia tarehe 17 hadi 21 Oktoba,2019 katika vituo 397 ambavyo ni vituo vyote vya afya katika Halmashauri zote za Mkoa wa Geita.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa