Na Hendrick Msangi
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ndugu Karia Rajabu Magaro Leo Septemba 30, amepokea Tuzo ya Mshindi wa Kwanza Katika Maonyesho ya Sita ya Teknolojia ya Madini yenye Kauli mbiu " Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi mazingira"
Maonyesho hayo yalifunguliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Dotto Biteko yamefungwa rasmi leo Septemba 30 na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman.
Wakipokea Tuzo hiyo kwa furaha, watumishi hao wameshukuru waandaji wote na Serikali kwa kufanikisha Maonyesho hayo na kupata ushindi huo. " Tumeshiri Maonyesho haya kwa vipindi vyote toka yameanzishwa na tumekuwa washindi wa pili mara mbili na washindi wa kwanza mara Nne, kwetu sisi ni furaha sana na tunapenda kuwakaribisha wawekezaji na wadau wote wa maendelo kuitembelea Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa ajili ya Fursa za maendelo, alisema Elexander Herman ambaye ni Afisa Maendelo Jamii wa Halmashauri Hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita inaishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuipatia fedha kwa ajili ya kufanikisha miradi ya maendelo
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa