Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeazimia kutumia mfumo wa GOTHOMIS katika vituo vyote vya Afya ifikapo Oktoba 30 mwaka huu,ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wagonjwa.
Maazimio hayo yamepitishwa na kikao cha Timu ya Halmashauri ya Usimamizi wa Huduma za Afya (CHMT) na Waganga Wafawidhi, kilichofanyika Septemba 2,2021, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Nzera.
Wajumbe wa kikao cha CHMT Wakijikabidhi kwa mwenyezi Mungu kupitia sala kabla ya kuanza kwa kikao
Mfumo huu unatumika kuorodhesha wagonjwa,kutunza taarifa zao,na kutoa majibu kwa njia ya mfumo, ili kudhibiti matumizi ya karatasi katika vituo vya Afya hasa Maabara.
Maazimio hayo yamepitishwa ikiwa ni hatua ya kukabiliana na changamoto za baadhi ya vituo vya Afya kutotumia vizuri mfumo huo, na vingine kutokuwa nao kabisa.
Wajumbe wa CHMT wakiendelea na kikao
Kwa matumizi ya mfumo wa GOTHOMIS ni dhahiri kuwa taarifa za mgonjwa kutoka kwa Daktari kwenda Maabara,kupokea majibu na kuchukua dawa, vyote vitaandikwa katika mfumo huo, hivyo kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kumbukumbu za mgonjwa, jukumu linalosimamiwa na Waganga Wafawidhi.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa