• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

Halmashauri ya wilaya Geita yakusanya mapato ya ndani kwa asilimia 122.6 kwa kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Posted on: July 28th, 2023


Na, Agrey Singo.

Halmashauri ya wilaya Geita imekusanya mapato ya ndani jumla ya shilingi 6,274,151,382.98 ambayo ni sawa na makusanyo ya asilimia 122.6 ikiwa ni jumla ya mapato yote yaliyokusanywa katika vipindi vya robo zote 4 (Julai 2023 – Juni 2023) za mwaka wa fedha wa serikali 2022/2023.

Hayo yamebainishwa katika taarifa ya kamati ya kudumu ya fedha, uongozi na mipango kwa kipindi cha aprili hadi juni 2023, iliyowasilishwa katika mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023, kilichofanyika Julai 28, 2023 kwa ajili ya kupokea taarifa za utekelezaji  wa shughuli za serikali ngazi ya halmashauri katika robo ya nne ya mwaka huo wa fedha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hadi kufikia mwezi Juni 2023, Halmashauri ya wilaya Geita ilikusanya kiasi cha shilingi 704,307,738.53 ikiwa ni mapato fungwa sawa na asilimia 120.62 ya makisio na shilingi 5,569,843,644.45 ikiwa ni mapato yasiyofungwa sawa na asilimia 122.36, ambayo imepelekea jumla mapato ya ndani kufikia shilingi 6,274,151,382.98 ambayo ni sawa na makusanyo ya asilimia 122.6.

Katika mapato hayo kiasi cha shilingi 1,820,802,623.60 kilihamishwa kwenda akaunti ya maendeleo kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

Aidha, kufikia mwezi Juni 2023, halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi 1,368,560,056 fedha za sequip kwa kwa kata za Isulwabutundwe na Ludete kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili za watumishi na shule mbili mpya.

Sambamba na hilo, taarifa hiyo imeongeza kuwa kufikia mwezi Juni 2023, halmashauri ya wilaya ya Geita ilipokea jumla ya shilingi 47,943,924,716.00 ikiwa ni ruzuku ya mishahara sawa na asilimia 76.60, shilingi 1,434,024,500.00 ikiwa niruzuku ya matumizi mengineyo sawa na silimia 110.07 ya makisio, shilingi 15,017,804,999.17 ikiwa ni ruzuku ya miradi ya maendeleo  sawa na asilimia 94.4 na shilingi 11.131,720,282.15 ilipokelewa nje ya bajeti.

Hivyo, jumla ya mapato yote yaliyopokelewa au kukusanywa ni shilingi 81,799,504,890.27 ambayo ni sawa na asilimia 96.52 ya makisio ya mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Akizungumza katika mkutano huo wa baraza la madiwani robo ya nne ya mwaka wa fedha 2022/2023, Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Mhe. Charles Kazungu amewapongeza waheshimiwa madiwani pamoja na watumishi wote wa halmashauri kwa usimamzi na ufuatiliaji uliopelekea kufikia mafanikio hayo makubwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Geita, Ndugu Karia Rajabu Magaro amewataka waheshimiwa madiwani na watendaji wa serikali kuzidisha ushirikiano ili kuendelea kufuatilia na kusimamia miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao pamoja na suala la ukusanyaji wa mapato.

Naye, mkuu wa wilaya Geita, Mhe. Cornel Magembe ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Geita kwa kufikia mafanikio hayo ya kukusanya mapato ya ndani kwa kuvuka lengo na kufikia asilimia 122.6 kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023 na kuwataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii na ushirikianoa kwa mwaka mpya wa fedha wa 2023/2024.



Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • DC KOMBA ARIDHISHWA NA UTEKEKEZAJI WA MIRADI KUELEKEA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

    May 06, 2025
  • MEI MOSI YALETA FARAJA KWA MAAFISA TARAFA GEITA.

    May 02, 2025
  • RC SHIGELA AIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WATUMISHI MKOANI GEITA.

    May 02, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI GEITA DC LAMPONGEZA MKURUGENZI MTENDAJI KWA KUPATA HATI SAFI

    April 30, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa