Mashindano ya UMISSETA ngazi ya Wilaya Msimu wa 2018/2019 yamehitimishwa kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya wasichana Nyankumbu, ambapo Geita DC imepata ushindi kwenye michezo ya mpira wa pete pamoja na riadha hata hivyo majirani zetu Geita TC wamepata ushindi wa jumla kwa kupata ushindi kwenye michezo ya mpira wa mikono kwa wasichana na wavulana, fani za ndani( ngoma na kwaya) huku Chato wakiibuka kidedea kwenye mpira wa miguu kwa wavulana na wasichana.
Katibu tawala wa Mkoa Denis Bandisa ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye ufungaji wa mashindano hayo, akijibu changamoto mbalimbali zilizohanishwa na Afisa michezo wa Mkoa Yesse Kanyuma ikiwemo upungufu wa walimu wa michezo, Bandisa amesema kuwa changamoto hizo zimeshaanza kufanyiwa kazi hivyo zitatatuliwa hazitojirudia katika mwaka ujao.
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita
Simu: +225 282520061
Mobile:
Barua pepe: info@geitadc.go.tz
Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa