• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Geita
Halmashauri ya Wilaya ya Geita

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
        • TASAF
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Maji
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
        • Utamaduni
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • UKIMWI
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
    • Viwanda
    • Biashara
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Uvuvi
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Ujenzi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe.Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha,Uongozi na Mipango
      • Uchumi,Ujenzi na Mazingira
      • Elimu,Afya na Maji
      • UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Wahe.Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Sheria ndogo
    • Mpango mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi/kitaifa
    • Hotuba za viongozi
    • Maktaba ya Picha

GEITA DC YAFANYA UZINDUZI WA PROGRAMU JUMUISHI YA TAIFA YA MALEZI,MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO- PJT-MMMAM

Posted on: February 1st, 2024

Halmashauri ya Wilaya ya Geita, imefanya uzinduzi wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya  Mtoto –PJT-MMMAM leo Februari Mosi, 2024.

Uzinduzi huo umefanyika makao makuu ya Halmashauri - Nzera ambapo Mgeni rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Karia Rajabu Magaro, amesema uzinduzi huo umefanyika ngazi hiyo ya Halmashauri yakiwa ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan  kupitia Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ambapo alielekeza programu hiyo izinduliwe ngazi zote kuanzia Taifa, Mkoa hadi Halmashauri.

Mkurugenzi Rajabu Magaro amesema uzinduzi huo ni mwendelezo wa baada ya uzinduzi ngazi ya Mkoa tarehe 21 septemba, 2023 na ngazi ya Taifa Desemba,2021.

Amesema program hiyo inalenga kukabiliana na kutokomeza changamoto zinazoonekana kuwa ni kikwazo cha “Hatua sahihi za ukuaji timilifu wa mtoto kimwili, kiakili na kijamii”.

“umri unaolengwa na program hii ni kuanzia umri wa miaka sifuri hadi miaka nane ambapo kwa mujibu wa tafiti za kisayansi imeonesha kuwa huo ndiyo umri nyeti wa kumtengeneza mtoto aliye bora au mtoto aliyedhaifu kimwili, kiakili na kijamii” alisema Karia.

Na kuongeza kwamba katika umri huo ubongo wa mtoto hupokea kile kinachoingia na mwili kujengwa kutokana na kile unachopatiwa.

Mkurugenzi Karia ametaja maeneo makuu matano ya msisitizo kwa ajili ya kuyazingatia wakati wa utekelezaji wa programu hiyo ambayo ni uzingatiaji wa huduma za afya bora kwa mtoto na mama ambapo kwa kufanya hiyo ni kutimiza adhma ya lengo namba 3 ya Maendeleo endelevu ya Dunia inayozungumzia Afya bora.

Eneo la pili,  Mkurugenzi huyo amesema ni lishe ya kutosha kwa mtoto na mama mzazi kuanzia akiwa mjamzito, na la tatu ni Malezi yenye Mwitikio.

Maeneo mengine amesema ni fursa za ujifunzaji wa awali na eneo la tano  ni ulinzi na usalama kwa watoto.

Maeneo hayo matano ya msisitizo katika utekelezaji wa programu hiyo, ni mwitikio wa Taifa katika utekelezaji wa malengo ya maeneleo endelevu ya Dunia –SDGs ambapo maeneo yote ya msisitizo ni utekelezaji wa malengo namba 2,3,4,na 16 ya SDGs.

Akizungumzia takwimu kuhusu malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto Mkurugenzi karia amesema Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa taarifa ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, inakadiriwa kuwa na jumla ya watu 936,302 ambapo wanaume ni 465,315, na wanawake ni 470, 987.

Kati ya watu wote hao, watu 199,697 sawa na asilimia 21% ni watoto wa umri wa chini ya miaka mitano (5).

Ambapo amesema takwimu hizo zinaashiria kuwa isipowekezwa kwenye malezi, makuzi na huduma sahihi kwa watoto basi Mkoa, Taifa na Bara la Afrika kwa ujumla litakabiliwa na changamoto kubwa ya kufikia maendeleo endelevu.

Hata hiyo ametoa rai kwa viongozi na wadau wakiwemo wa idara zote zinazotekeleza programu kuzingatia utekelezaji wa programu hiyo kwenye maeneo yao kupitia maelekezo na ushauri unaotolewa mara kwa mara.

Amewataka pia wakuu wa Taasisi na wadau wanaohusika na ulinzi na usalama wa mtoto kuweka mipangokazi ya kusaidia utengaji wa bajeti na kutoa fedha kwa utekelezaji.

Amewataka wadau wa vituo vya malezi kuhakikisha vinakuwa na madarasa yanayoongea, yaani madarasa ambayo yana vitendea kazi na vifaa yote ya kujifunzia kwa watoto wa awali.

Kwa upande wake Ummy Kileo, Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, amesema wataenda kusisitiza jamii kuzingatia lishe bora kwa mama mja mzito na hata baada ya mtoto kuzaliwa, ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mtoto kunyonyeshwa bila kula chochote kwa miezi sita.

Naye Afisa ustawi wa Jamii Jackson Chami amesema watoto wengi hawapati malezi bora ndani ya familia zao wawapo katika umri wa awali na kwamba changamoto kubwa ni kutokana na mifarakano ndani ya familia hivyo kupitia program hii, wazazi na walezi watapatiwa elimu ya namna ya kumuandaa mtoto ili kukabiliana na maisha yake ya baadae.

Mwalimu Pual Richard Magubiki ambae ni afisa Elimu Msingi, amesema katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita kuna shule za Msingi 246, na kila shule ina wanafunzi wa darasa la awali.

Amesema elimu ya awali ndiyo inayohusika zaidi na program hiyo, kwasababu imejikita kwa watoto wenye umri wa miaka sifuri hadi miaka 8, na kuongeza kwamba amefurahishwa nayo kwakuwa wamekumbushwa kuwa ubongo wa mtoto unaimarika zaidi ndani ya miaka sifuri hadi sita ambao ndiyo umri wa mtoto wa darasa la awali.

Amesema kutokana na program hiyo anatarajia kwamba ikitekelezwa kikamilifu walimu watapokea watoto ambao ubongo wao umeimarika, wanajitambua na wanajua namna ya kuyatawala mazingira,  jambo litakalowarahisishia walimu kuwafundisha stadi kuu tatu za kusoma kuhesabu na kuandika (KKK) kwasababu wazazi na walezi watakuwa wameshafanya kazi kubwa.

Ameongeza kutokana na program hiyo tayari Serikali kupitia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameshatoa fedha Shilingi 587,000 kwa ajili ya kuweka vifaa kwenye madarasa 37 ya elimu ya awali na tayari vimeshatengenezwa kwa ajili ya kuweka  mazingira mazuri kwa watoto hao kujifunzia.

Programu hiyo ya miaka mitano ilianza mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026 inatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wakiwemo mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kama NELICO kwa upande wa Geita.

Tangazo

  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA VIKUNDI January 23, 2025
  • TANGAZO LA KAZI GEITA DC September 10, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA September 16, 2024
  • Geita Mamlaka za Wilaya na malmaka za miji GP DOM.pdf September 16, 2024
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • UBORESHAJIWA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025 WAFIKIA KIKOMO GEITA.

    May 08, 2025
  • DC KOMBA ARIDHISHWA NA UTEKEKEZAJI WA MIRADI KUELEKEA MBIO ZA MWENGE WA UHURU 2025.

    May 06, 2025
  • MEI MOSI YALETA FARAJA KWA MAAFISA TARAFA GEITA.

    May 02, 2025
  • RC SHIGELA AIBUA MATUMAINI MAPYA KWA WATUMISHI MKOANI GEITA.

    May 02, 2025
  • Tazama zote

video

DED. WANGA AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA WANAOJIANDAA KUFANYA MITIHANI YA TAIFA
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Asili ya jina Geita
  • Fursa ya viwanda
  • Fursa ya madini
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA KATI, 2021
  • Vivutio vya Utalii
  • Miradi itakayotekelezwa
  • Miradi inayoendelea
  • Orodha ya wahe.Madiwani

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Bofya Hapa Kutuma,Kupokea na Kufuatilia Malalamiko,Mapendekezo,Maulizo na Pongezi Halmashauri ya Wilya ya Geita
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Watumishi Portal
  • Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS)
  • Ofisi ya Rais TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter Widgets

Ramani ya Sehemu

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Geita

    Anuani ya Posta: S.L.P 139 Geita

    Simu: +225 282520061

    Mobile:

    Barua pepe: info@geitadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Maswali na Majibu yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Eneo
    • Huduma

Hakimiliki@ Halmashauri ya wilaya ya Geita , Haki zote zimehifadhiwa